Na Bakari Mwakangwale

JUMUIYA ya Wanataaluma wa Kiislamu Tanzania (TAMPRO), inatarajia kufanya Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa viongozi wapya wa Kitaifa, sambamba na kutoa sura mpya ya kiutendaji.

Sheikh Kichwabuta, aongoza harambee

Ni ya ujenzi wa kituo cha Afya Nyanga

Kuanza kutoa huduma za Afya kabla ya 2022

 

Na Bakari Mwakangwale


KITUO cha Afya chenye hadhi ya Hospitali, Nyanga Islamic Health Center, kinachojengwa Wilayani Bukoba, kinatarajia kuanza kutoa huduma za Afya mwishoni mwa mwaka huu 2021.

Hayo yamebainika katika Harambee ya Uchangiaji wa Kituo hicho cha Afya iliyofanyika Agosti 14, 2021, katika viwanja vya Hospitali hiyo iliyopo Kata ya Nyanga, Manispaa ya Bukoba, Mkoani Kagera.

Harambee hiyo ilikwenda sambamba na Tamasha la siku mbili lililoanza Agosti 13, 2021, ambapo Waislamu na wadau mbali mbali wa ndani na nje ya Mkoa wa Kagera, walikusanyika na kufanya kazi mbalimbali za mikono.

Ujenzi huo wa Kituo cha Afya cha Kiislamu ambacho kimekuwa maarufu kama Nyanga Islamic Health Center, licha ya kujegwa kwa nguvu za Waislamu kipo chini ya Taasisi ya Umoja wa Maendeleo ya Wanawake wa Kiislamu Kagera (UMWAKIKA), huku wadau mbalimbali wakitakiwa kuendelea kuunga mkono ujenzi huo kwa kuchangia fedha au vifaa vya ujenzi.

Jumla ya Shilingi Milioni 3.3, Tasilimu zilipatikana katika Harambee hiyo iliyoongozwa na Sheikh wa Mkao wa Kagera Sheikh Haruna Kichwabuta, pesa ambayo itaendeleza Ujenzi wa Kituo hicho.

Imeelezwa kuwa kiasi cha Shilingi Milioni Mia moja, zinahitajika ili Kituo hicho cha Nyanga Islamic Health Center, kikamile ambapo kitatoa huduma kwa Wananchi wa Dini zote.

Akiongea na Waislamu katika viwanja vya Hospitali hiyo, Sheikh Kichwabuta alisema kama Waislamu wanataka kupata maendeleo ni lazima wawe kitu kimoja haswa katika masuala ya kimaendeleo yanayogusa jamii ya Kiislamu pasina kujali madhehebu yao.

Alisema, mara nyingi shughuli za kimaendeleo za Waislamu zinakwamishwa na Waislamu wenyewe kutokana na kutokuwa kitu kimoja, akasema na wale wanaobaki nyuma katika maendeleo ni sawa na wale waliokasirikiwa na Mtume (s.a.w) wakati wa Vita ya Jihad.

Ili kuendana na kasi ya maendeleo na kuondokana na dhana ya utegemezi, Sheikh Kichwabuta, alisema Waislamu ni lazima wawe kitu kimoja ili kushilikiana kufanya shughuli za Kimaendeleo ikiwemo miradi mbalimbali ya kijamii.

 

 

Group Khairat watoa msaada magereza Handeni, Maweni

Na Bint Ally Ahmed

Baraza Kuu la Wanawake wa Kiislamu  Tanzania,  kupitia kundi la kina mama la mtandao wa Whatsup lenye anuani ya Groups Khairat, wametoa msaada wa chakula  chenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni moja na laki tano (1,500,000) kwa wafungwa na mahabusu wanaotumikia vifungo vyao katika gereza la Handeni na gereza la Maweni Jijini Tanga, mwishoni   mwa wiki iliyopita.

 Baraza Kuu la Wanawake wa Kiislamu  limekuwa linafanya kazi  kubwa ya kuwaunganisha wanawake wa Kiislamu nchini,  linaloongozwa na Ukht. Fatma Ally Chitapa, ambaye pia ndiye kiongozi wa group hilo, limekuwa likiwaelimisha kina mama juu ya dini yao na dunia pia,  lakini pia wamejikita kwenye malezi bora ya Kiislamu kwa kuwa mwanamke ndio msingi na nguzo ya familia.

 Ukht. Fatma, amesema kuwa kundi lake la Whatsup linalotokana na Baraza Kuu la Wanawake wa Kiislamu hapa nchini,  wamekuwa wakijihusisha na kusadia wahitaji mbalimbali kama vile vituo vya watoto yatima na wale wenye uhitaji maalumu na kutekeleza kazi zake mbalimbali za masuala ya kidini kwa kipindi kirefu.

Ukht. Fatma, ameongeza kuwa wamekabidhi  chakula hicho kwa Mkuu wa gereza la  Maweni,  Revocatus Kessy, mchele kilo 300, mafuta ya kupikia lita 60, sabuni boksi  kubwa moja, Misahafu ya Tafsiri pamoja na vitabu mbalimbali vya mafundisho ya dini ya Kiislam.

 Baadae walikabidhi chakula hicho kwa Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza  Anthony Mbogo, kupitia kwa Mkuu wa Gereza la Handeni

mchele Kilo 200, mafuta ya kupikia lita 40, Sabuni boksi kubwa moja, Misahafu ya Tafsiri pamoja na vitabu  mchanganyiko vya mafundisho ya Uislamu.

 Aidha wafungwa hao nao walipata fursa ya kutoa neno la shukrani kwa wanawake hao na kujiona ni miongoni mwa watu wanao kumbukwa na jamii ya uraiani.

Group Khairat limekuwa likifanya kazi  mbalimbali za kheri kwa kuchangishana kidogo walicho nacho na kukifikisha kwa wahitaji.

Kwa kuzingatia umuhimu wao wa kutoa kile walicho jaaliwa na Mola wao, kikundi hicho kila wanapoona kuna shida au uhitaji eneo fulani, huchangishana pesa na kuzipeleka pale wanapoona kuna uhitaji.

 Mkuu wa gereza  la Handeni, Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza  Anthony Mbogo na mahabusu walitoa shukran zao za dhati kwa sadaka hiyo waliyoipokea  kutoka kwa kina mama hao.

Alisema wafungwa na mahabusu  pamoja na watumishi wenzake wanashukuru kwa kile kilichotolewa kwa ajili ya wafungwa.

Mkuu huyo wa gereza aliomba ushirikinao katika kutatua changamoto nyingine  kama hizo.

 Kwa upande wa  Mkuu wa Magereza Wanawake Maweni, Upendo Kazumba, aliwashukuru kina mama hao kwa moyo wao wa kujali na kutoa walicho nacho kwa ajili ya wahitaji na kuwaomba kutowasahau  hata kwa kidogo walicho nacho, kwani kutoa ni moyo na sio utajiri.

Msaidizi wa Kikundi hicho  cha wanawake Ukht. Mayasa Sadalla, amesema kikundi kimetoa  msaada huo kwa wafungwa wa gereza la Handeni na Maweni, Tanga kwa kuona kuwa wana jukumu la kuwakumbuka ndugu zao, hasa wathirika wa kesi za ugaidi wanaoshikiliwa  mahabusu kwa muda mrefu sasa.

Ukht. Mayasa,  amesema kuwa  Baraza la Wanawake  wa Kiislamu kupitia group la  Khairat,  waliguswa na kuona wana wajibu kufanya kila namna kuwasaidia wafungwa  kwa kutoa walicho nacho, kwani kutoa ni moyo na kwa Allah hakuna kidogo.

 Naye Ukht Fatma, amewaomba Waislamu kulikumbuka  kundi hili la watu walioko magerezani, kwani wao wamesahaulika sana na jamii. 

Kama una sadaka yako iwe ni magodoro, nguo za wanaume na wanawake, sabuni, mafuta kula, vitabu vya dini ya Kiislamu na mahitaji mengine muhimu ya mwanadamu na  unahitaji kuifikisha kwa makundi mbali mbali yanayohitaji, unaweza kuwapigia kina mama hao wanao jishughulisha na mambo mbalimbali ya kheri katika jamii.

 Wasiliana na Ukht. Fatma kwa namba hii 0712 326 612.

                             

Na Bint Ally Ahmed

Taasisi ya Udugu Social Help Welfare yenye Makao Makuu yake Buguruni Jijini Dar es Salaam imefanikisha nia na matamanio yake ya kuwafariji yatima wa kituo cha Al-Azam kilichopo Mbagala, kwa kujumuika  na watoto hao pamoja na walezi wao kwa kupata

Aidha, Taasisi hiyo imetoa wito kwa wadau kuendelea kuwakumbuka na kuwajali yatima na watoto wanaoishi katika mazingira magumu popote walipo, kwani bado wanazo changamoto nyingi zinazohitaji ufumbuzi.

Akizungumza mara baada ya kupata chakula cha mchana na yatima hao, mratibu wa kundi hilo lenye wanachama zaidi ya 20, Hajat Neema Maumba amesema kilichowasukuma kushiriki chakula pamoja na yatima ni kuwafariji, wasijione wapweke katika maisha yao kwa kukosa malezi ya wazazi wao.

Amesema, ni utaratibu wao wa kila mwaka kushiriki chakula na watoto yatima na wamekuwa wakifanya hivyo katika maeneno mbalimbali katika jiji la Dar es Salaam.

Amesema taasisi yao ya Udugu Social Help Welfare sio ya kidini, lakini wengi wao ni Waislamu, na kwamba wanasaidia watu mbalimbali bila kujali dini zao.

“Sisi tunaitwa Udugu Social Help Welfare, tupo Buguruni Malapa, tuko wakina mama 20, tulianza mwaka 2009, tumekuwa tukisaidia watu wenye mahitaji sehemu nyingi na bado tunaendelea kufanya hivyo,” alisema kioongozi huyo.

“Tumesikia changamoto watoto hawa wanazokutana nazo katika kituo hiki, baada ya watoto kueleza changamoto zao, tunamuomba Mwenyezi Mungu atuwafikishe tuweze kusaidiana”, amesema Hajjat Neema.

Amesema kuwa wametoa msaada kwa watoto hao jumla ya vitu vyenye thamani ya shilingi laki sita na elfu sitini na nane (668,000) msaada uliotoka mifukoni mwao kwa kuchangishana kila mwezi.

Hajjat Neema amewataka Waislamu, hasa kina mama kuwakumbuka wenye uhitaji maalumu kwa kuwasaidia na kuwapa faraja kuwahurumia na kuona wao ni sehemu ya jamii.

“Watoto kama hawa wanahitaji ukaribu wetu, hivyo kushirikina nao ni kuwapa upendo ambao nao kama wanaadamu wanauhitaji sana,” amesema Hajjat Neema.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa taasisi ya kulelea watoto yatima na wenye mazingira hatarishi cha Al-Azam Orphanage Center Sheikh Musa Chele ametoa wito kwa wafadhili kuacha kuwatumia watu wa kati kufikisha sadaka zao katika makao ya watoto yatima.

Amesema, kwa muda mrefu watu hao wa kati (Agent) wamekuwa wakitumia fursa hiyo vibaya kwa kujinufaisha wao wenyewe badala ya watoto yatima.

Akielezea historia ya kituo chao, Sheikh Musa alisema Kituo chao kimeanzishwa mwaka 2009 kikiwa na watoto 10, wavulana 5 na wasichana 5, hadi kufika mwaka 2021, walikuwa na watoto 60, kati yao wanawake 35 na wanaume 25.

45 kati ya watoto hao 60, wanaishi katika Kituo na wengine wanalelewa wakiwa majumbani mwao.

Amesema Kituo kinakabiliwa na changamoto nyingi, lakini kubwa ni huduma za afya, watoto wengi hawana bima za afya ili kuwasaidia kupata matibabu bila hofu.

Pia amesema kuna changamoto ya rasilimali fedha za kulipa pango la nyumba, ada za wanafunzi, na chakula, kwa mwezi wanalipa shilingi 300,000 fedha ambazo ni nyingi kwa uwezo wao.

Upande wa mafanikio amesema, Kituo kimeweza kununua kiwanja na kuwaomba wadau kuwajengea nyumba ili watoto wakaishi huko na kuepukana na adha ya kupanga.

 

"TUNAFANYAJE Ustadh kuhakikisha akina mama wa Kiislamu wanauishi Uislamu?"

"Ustadh tunafanyaje ili mabinti zetu wawe salama kiimani..."?

Hili ndilo jambo la mwanzo ambalo Ukhty Nadhira angekuuliza punde ukikutana nae. Innaa lillaahi wa innaa ilayhi raajiuun. Amerejea kwa Mola wake, Alhamdulillaah! Ametekeleza wajibu wake na amefikisha ujumbe.

Kwa mara ya kwanza nakutana nae akiwa ni mwanafunzi wa program ya kuwaandaa Walimu wa EDK kwa Madrasa na Shule za Msingi mwaka 2006 wakati huo tayari ni mama wa watoto watatu. Mpaka wakati huo Ukhty Nadhira alikuwa mzoefu kwenye harakati za kuelimisha akina mama na mabinti wa Kiislamu, lakini kila aposikia panasomeshwa, basi alikuwa tayari kuwa mwanafunzi; kwa takriban wiki 30 hivi tulikuwa nae kama mwanafunzi. Hakuishia kuwa mwanafunzi bali alihamasisha wenzake kuwa wanafunzi na akawa mwalimu wao.

Kwa kuthanini program ile, Ukhty Nadhira aliianzisha katika Madrasa Rahman Kinyerezi mahali ambapo palikuwa ndio Kituo cha cha harakati, wakikutana akina mama na kujifunza Uislamu na kulea mabinti zao kiakili na kiroho. 

Ukhty Nadhira mbunifu wa program za kimalezi, muanzilishi na msimamizi, amewalea vijana wengi wa kike na wa kiume kupitia Daarul Uluumi Kariakoo ambapo palikuwa pakiendeshwa semina mbali mbali za kimalezi kwa vijana na wanafunzi wa Kiislamu kidato cha kwanza hadi cha sita na wanufaika wa program ile waliendelea kuhudhuria hata walipokuwa vyuoni!

Ukhty Nadhira alihamasisha, kusimamia na kushiriki makongamano ya akina mama wa Kiislamu kimkoa, kikanda na kitaifa akishirikiana na akina mama wengine wa Kiislamu. Tija ya makongamano haya ni pamoja na uwepo wa madrasa hai za akina mama na mabinti wa Kiislamu, uwepo wa shule za awali katika madrasa nyingi na kutoa ajira kwa vijana waliosomea ualimu.

Huwezi kumtaja Ukhty Nadhira kwamba alikuwa tajiri kuweza kuyafanya yote haya, lakini alijaaliwa uwezo wa ku-mobilize rasilimali na kuzielekeza zinapostahiki hivyo kujenga Imani ya kuaminiwa na kukabidhiwa amana bila tone la shaka.

Tunamuadhimishaje Ukhty Nadhira? 

Ukhty Nadhira alikuwa mpole sana kwa watu lakini mkali inapokuja jambo la Uislamu na Waislamu. Alikuwa mwenye msimamo akisimamia kile anachokiamini. Hakuwa mtu rahisi wa kukata au kukatishwa tamaa. Akipanga jambo lake muda wa kuwa anaamini yupo sahihi na lina tija kwa Uislamu na Waislamu, hachelei kubakia na watu wachache.

Alikuwa hodari mno wa kuwatia watu moyo na kuwapa bishara njema. Mwepesi kusaidia mwenye sikio makini na moyo laini. Aghalabu shida za watu wengine alizifanya zake.

Ameacha alama katika maisha ya akina mama na vijana wa kike na wakiume na kwa kila Imam na mwalimu wa madrasa aliyeshirikiana naye. Ni wajibu wetu kuendeleza pale alipoishia na kuongeza hima zaidi katika yale aliyoyafanya.

 “Hao ni watu waliokwisha pita. Wao watapata waliyo yachuma, na nyinyi mtapata mliyo yachuma, wala hamtaulizwa nyinyi yale waliyo kuwa wakifanya wao.” (2:141)

Allah Ampe Kauli thabiti. Amrehemu na Amsamehe makosa yake.

 

Abu Sumayyah Salah

 

Na Bint Ally Ahmed

Waislamu wametakiwa kushukuru kwa kuachiwa huru Masheikh 36 wa Uamsho waliokuwa wakishikiliwa katika Gereza la jiji la Dar es Salaam, lakini wakatakiwa kuongeza

harakati za kupigania haki za idadi kubwa ya Waislamu na Masheikh wanaoendelea kushikiliwa kwa muda mrefu sasa katika magereza mbalimbali nchini.