Na Bint Ally Ahmed

Ikiwa ni wiki moja imepita tangu Taasisi ya Al-Firdaus kuzindua Msikiti wa kisasa Sharif Shamba Wilaya ya Ilala wenye thamani ya milion 220, taasisi hiyo imezindua Msikiti mwingine Kimara Mwisho Wilaya ya Ubungo eneo Michungwani wenye thamani ya shilingi milioni 150.

Ndani ya wiki mbili taasisi hiyo imezindua Misikiti miwili yenye jumla ya thamani  ya shilingi milioni 370, fedha za wanachama wake.

Uzinduzi huo umekuja kufuatia kukamilika kwa ujenzi wa Msikiti huo uliogharamiwa na wanachama wa Al-Firdaus Charitable Foundation, yenye makao yake Makuu  jijini Dar es Salaam.

Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa Msikiti huo, Imam Mkuu wa Msikiti huo Ustaadh Fikiriani Mlawa, alisema changamoto iliyobaki ni Msikiti huo kujaa waumini na kuleta tija.

Akizungumzia mwamko wa waumini wa Kimara Michungwani juu ya dini yao, Ustaadh Mlawa, alisema wengi wamehamasika na dini yao .

“Mara nyingi kipimo kikubwa cha mwamko wa waumini katika eneo husika ni swala ya fajri, kwetu Alhamdullah tunajaza swafu kadhaa, ni matumaini yangu baada ya kukamilika Msikiti huu watu wataongezeka,” alisema.

Ustaadh Mlawa aliongeza kuwa Msikiti huo umekuja wakati muafaka ikizingatiwa kuwa mwezi mtukufu wa Ramadhani iko karibu ambako kunakuwa na ongezeko la waumini.

“Tunamuomba Mungu atupe mwongozo wa kusimamia Msikiti huu uwe kwenye hali nzuri, tunatarajia kuwa na darsa za kufundisha waumini kujua jinsi ya kumuabudu Allah, kujua jinsi ya kuamiliana na mambo yenye mfano na hayo.

 

Kwa upande wake Imam wa Msikiti wa Muumin Islamic Center uliopo vyumba Vinane, Sheikh Hassan Jida, ambaye alifika kwenye uzinduzi huo akiwa ni miongoni mwa wageni waalikwa. aliwaasa waumini kupupia kheri zinazopatikana ndani ya Msikiti huo.

Alisema Msikiti ndio bahari ya elimu na ndio sababu hata Mtume Muhammad (saw) alipofika Madina, kitu cha kwanza kukifanya ni ujenzi wa Msikiti uliotoa wasomi wakubwa walioupeleka Uislam mbele.

“Tupo hapa katika Msikiti wa Al-Mustafa, lengo ni kushuhudia ufunguzi wa wake ili watu waweze kufanya ibada zao za kumtukuza Allah, Ramadhani ipo karibu tunaamini watu watafurika l kuja kufanya ibada zao,” alisema Imam Hassan.

Hata hivyo ameonya wale wenye nia ya kufanya magomvi waachane na tabia hiyo kwani Msikiti ni kituo cha amani, inapaswa watu wajihisi wana amani wanapoingia kufanya ibada zao

 

“Misikiti ni mali ya Allah, wajane, wayatima na watu wenye uhitaji hapa ni nyumbani kwao, badala ya kufikiria kupata uongozi wajikite katika kuwafahamu watu wao, wajane wangapi, yatima wangapi waweze kuwasaidia,” alifafanua.

Awali, akizungumza na waandishi wa habari, Katibu wa Taasisi ya Al-Firdaus Charitable Foundation Saleh Al-hinai alisema Msikiti wa Al- Mustafa umejengwa kwa gharama ya shilingi Milion 150.

Kuhusu malengo ya kujenga misikiti zaidi, Katibu Saleh alisema Taasisi hiyo itaendelea kujenga misikiti pamoja na kutoa misaada ya kijamii lengo likiwa ni kutafuta radhi za Al