Na Bakari Mwakangwale

MAUAJI dhidi ya Waislamu yanayotokea katika nchi nyingi hivi sasa, yanatokana na chuki, wengine wakiita ‘Islamphobia’

Hayo yamesemwa na Amir wa Shura ya Maimamu Wilaya ya Kinondoni, Ustadhi Mzee Mwinyikai, akiwahutubia Waislamu katika ibada ya swala ya Ijumaa ya wiki iliyopita katika Msikiti wa Mtambani, Jijini Dar es Salaam.

Katika Khotba yake hiyo, Ustadhi Mwinyikai, amezungumzia kwa kina juu ya mauaji ya Waislamu yanayofanywa mara kwa mara katika nchi mbalimbali Duniani.

Akirejea tukio la kuuwawa Waislamu 50, na wengine kadhaa kujeruhiwa katika Misikiti miwili nchini New Zealand, alisema tukio hilo limewakumbusha Waislamu nchini matukio kama hayo ya kupigwa na kuuwawa kwa risasi Waislamu wakiwa Msikiti.

Alisema, ukirejea mauaji ya New Zealand ni mtindo na staili ileile hali inayotokana na ugonjwa uliowaingia maadui wa Uislamu unaoitwa ‘Hofu juu ya Uislamu.’

Hivyo, wanajaribu kuzima Nuru ya Uislamu inayokuwa kwa kasi katika nchi mbalimbali Ulimwenguni.

Akasema, Waislamu wanatakiwa kuelewa kuwa yanayojiri dhidi yao na Uislamu kwa ujumla yanadhihirisha maneno ya Mwenyezi Mungu katika Qur’an, pale alipowataja Mayahudi, Manaswara na mfano wa hao kuwa hawatokuwa radhi mpaka Waislamu wafuate mila zao.

Akawataka Waislamu nchini kutokata tamaa badala yake washikamane katika Dini ya Mwenyezi Mungu kwa juhudi na nguvu kubwa zaidi