Na Bint Ally Ahmed

Amana bank wamesini mkataba na Taxfy Hapa nchini wa kuwawezesha madereva wa  Taxify kumiliki vyombo vya moto  (Motor Vehical Financing scheme).

Hayo yamesemwa na Dasu Mussa, Meneja Mkuu wa Biashara wa Amana Bank alipokuwa akiongea na waandishi wa habari wakati wa kusaini mkataba na  kampuni ya   taxfy hapa nchini Nov 5, mwakka huu katika ukumbi wa Mikutano Serena jijini Dar es salaam.

Bwaan Dasu amesema kuwa lengo kuu la amana ni kuboresha usafiri na kuwaongezea kipato  kwa kuwawezesha madereva hao kumiliki vyombo vyao vya moto wenyewe.

Dasu Amesema kuwa amana bank ni benk inayoendeshwa kwa kuzingatia misingi ya kiislam hatua hii ni sehemu ya mikakati ya kuifanya benki hii kuwa kiongozi katika kutoa huduma  za ubunifu zinazolenga kuinua jamii kiuchumi.

Aidha amesema kuwa uwezeshaji huu utafanyika katika vikundi, hivyo madereva madereva  watahitaji kuunda kikundi cha madereva kumi ambao watadhaminiana wenyewe.

Dasu amefafanua kuwa dereva ataweka amana isiyopungua 10% ya thamani ya chombo cha moto anachohitaji kuwezeshwa, amana  hii itatumika kama dhamana mpaka  dereva  atakapomaliza kufanya marejesho.

Aidha amesisitiza kuwa dereva atafanya marejesho kulingana na makubaliano na benk katika kipindi kisichopungua miaka miwili.

Aidha dasu amesema kuwa benk ya amana itazingatia vigezo mbali mbali katika uwezeshaji huu ikiwemo dereva kuwa na uzoefu wa kutosha na rekodi nzuri.

Kwa upande wa taxfy Tanzania Remmy Eseka,  meneja wa taxfy Tanzania, amesema kuwa Taxfy ni kampuni ya kimataifa ya usafirishaji kwa njia ya mtandao na wana matawi katika nchi 25 dunuani wanafanya kazi hii ya usafirishaji.

Bwana Remmy amesema kuwa wao wanaendesha vyombo vya moto ambapo kwa sasa wanatoa huduma hiyo ya usafiri kwa mikoa mitatu mikoa hiyo ni Dar es salaam, Dodoma, na Mwanza, na wana taxi, bajaji. Katika mikoa hiyo  mitatu.

Amesema kuwa wao wanashukuru sana kwa Amana Bank kuwaamini na kuona wanaweza kufanya kazi pamoja na kuwawezesha madereva wao kuweze kumiliki magari yao wenyewe.

Remmy Amesema kuwa wao wanatoa ajira kwa vijana kwani ili kujiunga na Taxfy lazima uwe umejiunga na kampuni yao na vielelezo vyote viko katika kampuni yao hivyo inasaidia kukufanya mteja uwe salama katika safari yake.