Kufuatia tishio la kufyatua risasi shuleni, Polisi ya Marekani imetangaza hali ya hatari katika shule 19 za jimbo la Colorado..

Polisi inamtafuta binti mmoja mwenye umri wa miaka 18 kwa jina la Sol Pais, ambaye ametoa matamshi ya kutishia kufyatua risasi katika shule za jimbo hilo.

Imesema kutokana na kutoeleweka vyema shule inayolengwa katika tishio hilo, Polisi wameamua kufunga kwa muda shule ya sekondari ya Columbine na shule nyingine 18 katika jimbo hilo.

Aprili 20, 1999 wanafunzi wawili katika shule hiyo walifyatua risasi kiholela na kuwaua wanafunzi wenzao 12 na mwalimu mmoja.

Upelelezi wa Polisi wa FPI ulimesema kuwa mwanafunzi Pais, alifika jimboni hapo majira ya usiku siku ya Jumanne na kwamba tayari alikuwa ameandaa silaha.

Pais aliwasili katika mji wa Denver, ambao ni mji ulio na wakazi wengi zaidi jimboni hapo na kutoa matamshi ya vitisho, lakini hakusema ni shule gani angeishambulia.

Kila mwaka maelfu ya watu katika pembe tofauti za Marekani hupoteza maisha au kujeruhiwa kutokana na ufyatuaji risasi.

Ushawishi wa kambi zenye nguvu za utengenezaji silaha katika serikali na Kongress ya Marekani umevuruga juhudi zote zinazofanywa na makundi ya kutetea haki za binadamu zinazolenga kubuniwa sheria kali za kudhibiti umiliki wa silaha nchini humo.parstoday