Ukurasa wa Twitter wa chama cha Kisoshalisti cha Sweden, ambacho ni mshirika mkuu wa serikali ya nchi hiyo, umetumika kusambaza ujumbe unaotaka Waislamu wauawe.

 

Hata hivyo taarifa za chama hicho zilieleza kuwa Ukurasa wake wa Twitter wa chama hicho cha Kisoshalisti ulidukuliwa na wadukuzi wabaguzi.

Baada ya udukuzi huo katika ukurasa huo ukawekwa ujumbe unaotaka Waislamu wote wauawe.

Katika taarifa iliyotolewa na chama hicho ilisema kuwa ukurasa wa chama hicho wenye wafuasi wapatao 850,000 ulidukuliwa kuanzia majira ya saa 8:00 na wadukuzi wabaguzi na ilipofika saa 3:30, saa za nchi hiyo waliweza kuumiliki tena ukurasa wao.

Wadukuzi hao wabaguzi walichapisha habari mbalimbali katika ukurasa huo, ikiwamo inayotaka Waislamu wote wauawe, habari nyingine ni ile iliyosema Waziri Mkuu wa Sweden na kiongozi wa chama cha Kisoshalisti Stefan Löfven, amejiuzulu wadhifa wake na ameanza kufanya kazi jeshini kama Luteni.

Habari nyingine iliyochapishwa katika ukurasa huo ni inayohusu biashara ya dawa za kulevya kuruhusiwa.

Msemaji wa chama Åsa Söderén, alisema kwamba ujumbe hizo hazina uhusiano wowote na chama hicho na kwamba, wamefungua kesi ya jinai kuhusiana na tukio hilo. Parstoday