Urusi yapeleka msaada Venezuela

Urusi imetuma zaidi ya wanajeshi 100 na tani 35,000 za vifaa vya matibabu nchini Venezuela.

Kwa mujibu wa habari, Urusi imetuma msaada huo nchini Venezuela kwa kutumia ndege zake za kijeshi.

Kulingana na vyombo vya habari nchini Urusi, ndege ya kijeshi ya Urusi imetua katika uwanja wa ndege wa Simon Gaudi, katika mji mkuu wa Caracas Kaskazini mwa Venezuela.

Ndege hiyo ilikuwa imebeba zaidi ya wanajeshi 100 wa Urusi na tani 35,000 za vifaa vya matibabu kwa ajili ya kuisaidia Venezuela.

Hakuna maelezo zaidi yaliyotolewa na mamlaka za nchi hizo mbili.

Hata hivyo hapo awali Rais wa Venezuela Nicolas Maduro, alitangaza kuwa nchi yake itapokea msaada kutoka Urusi.

Ripoti zinaonyesha kuwa Venezuela inapata wakati mgumu kupata chakula hasa unga.

Wananchi wamekuwa wakisubiri kwa muda mrefu kabla ya kupata huduma ya chakula, hasa katika maduka yanayomilikiwa na serikali.

Hali mbaya ya kiuchumi nchini humo imesababisha maandamano ya muda mrefu na wananchi wanamtaka Rais Maduro atoke madarakani jambo ambalo linaonekana sio rahisi.

Juan Guaido, Spika wa Bunge la Venezuela alijitangaza kuwa Rais wa mpito na kutambuliwa na utawala wa Marekani, Australia, Canada, Colombia, Peru, Ecuador , Paraguay, Brazil, Chile, Panama, Argentina, Costa Rica, Guatemala na Bunge la Ulaya.

Uturuki, Mexiko, Urusi, Iran, Cuba, China na Bolivia zinamuunga mkono Rais Nicolas Maduro.

Maduro amekata mahusiano ya kidiploamsia na nchi ya Marekani, huku Rais Trump akitoa vitisho vya kuwa huenda Marekani ikaiingilia Venezuela kijeshi kama njia ya kuutatua mgogoro huo.

Vyombo vya habari nchini Venezuela vimeripoti kwamba askari hao walipokelewa na viongozi wa ngazi ya juu wa kijeshi wa Venezuela pamoja na ubalozi wa Urusi nchini humo katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Simón Bolivar.

Aidha vyombo hivyo vya habari havikuashiria lengo kuu la ujumbe huo wa kijeshi wa Urusi au kilichomo kwenye shehena ya misaada hiyo.

Kutangazwa habari ya kutumwa ndege hizo za misaada kutoka Urusi, kumejiri baada ya Juan Guaidó, kiongozi wa upinzani aliyejitangaza kuwa Rais wa Venezuela kudai kwamba, Rais Nicolás Maduro wa nchi hiyo amekosa uungaji mkono wa ndani na kimataifa.

Katika wiki za hivi karibuni Marekani sambamba na kutangaza kumuunga mkono Guaidó, imedaiwa kufanya pia njama za kutekeleza mapinduzi ya kijeshi dhidi ya Rais Maduro aliyechaguliwa na wananchi.

Kabla ya hapo pia, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ilitangaza kuwa tayari kutuma misaada ya dawa na vifaa vya tiba nchini Venezuela.

Juan Guaidó alijitangaza kuwa Rais wa muda wa Venezuela Januari 23 mwaka huu kupitia uungaji mkono kamili wa Marekani na washirika wa Washington.

Hata hivyo licha ya njama hizo za kutaka kumuondoa madarakani Rais Maduro, jeshi na wananchi pamoja na nchi kama vile Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Urusi, China na mataifa kadhaa ya dunia yameendelea kusisitizia ulazima wa kuheshimiwa haki ya kujitawala nchi hiyo ya Amerika ya Latini.trt.net.tr/Parstoday.

  Ndege mbili za Urusi zilizobeba tani 35,000 za misaada zimetua mjini Caracas, mji mkuu wa Venezuela.

Mbali na misaada hiyo, ndege hizo zimewashusha pia karibu askari 100 wa Russia.