Baada ya kupita miezi sita, sasa ndipo serikali ya Marekani imeamua kutekeleza marufuku ya kuingia nchini humo raia 16 wa Saudi Arabia wanaotuhumiwa kuhusika katika mauaji ya mwandishi wa habari mkosoaji, Jamal Khashoggi.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani imetoa taarifa kwa vyombo vya habari na kusema kuwa, baada ya kuridhika na ushahidi unaothibitisha kuhusika raia hao 16 wa Saudi Arabia katika ukatili dhidi ya haki za binadamu, serikali ya Marekani imeamua kuwapiga marufuku kuingia nchini humo wao na jamaa zao wa karibu.

Jina la Saoud al Qahtani, Mshauri Mkuu wa Mohammad bin Salman, mrithi wa kiti cha ufalme wa Saudi Arabia ambaye ni miongoni mwa watuhumiwa wakuu wa mauaji ya Khashoggi limo kwenye orodha hiyo.

Hivi karibuni, polisi ya kimataifa Interpol ilitoa hukumu ya kutiwa mbaroni popote atakapopatikana.

Tarehe pili Oktoba 2018, timu ya mauaji ya serikali ya Saudi Arabia ikiongozwa na al Qahtani, ilifanya mauaji ya kutisha dhidi ya Jamal Khashoggi, aliyekuwa akiukosoa uongozi wa hivi sasa wa Saudia. Mauaji hayo ya kinyama yalifanywa na timu hiyo ya wauaji 15 wa Saudi Arabia ndani ya ubalozi mdogo wa nchi hiyo mjini Istanbul Uturuki.

Mashirika mbalimbali ya kijasusi, likiwemo Shirika la Kijasusi la Marekani CIA yametoa ripoti zao na kusisitiza kuwa amri ya kuuawa Khashoggi ilitolewa na bin Salman mwenyewe, mrithi wa kiti cha ufalme wa Saudi Arabia.

Hata hivyo serikali ya Donald Trump ya Marekani imekataa katakata kukata uungaji mkono wake kwa bin Salman licha ya kukiri kwamba maafisa wa serikali ya Saudi Arabia ndio waliomuua kikatili Khashoggi.parstoday.

.

Latest News

Most Read