Na Bint Ally Ahmed

Taasisi ya Udugu Social Help Welfare yenye Makao Makuu yake Buguruni Jijini Dar es Salaam imefanikisha nia na matamanio yake ya kuwafariji yatima wa kituo cha Al-Azam kilichopo Mbagala, kwa kujumuika  na watoto hao pamoja na walezi wao kwa kupata

Aidha, Taasisi hiyo imetoa wito kwa wadau kuendelea kuwakumbuka na kuwajali yatima na watoto wanaoishi katika mazingira magumu popote walipo, kwani bado wanazo changamoto nyingi zinazohitaji ufumbuzi.

Akizungumza mara baada ya kupata chakula cha mchana na yatima hao, mratibu wa kundi hilo lenye wanachama zaidi ya 20, Hajat Neema Maumba amesema kilichowasukuma kushiriki chakula pamoja na yatima ni kuwafariji, wasijione wapweke katika maisha yao kwa kukosa malezi ya wazazi wao.

Amesema, ni utaratibu wao wa kila mwaka kushiriki chakula na watoto yatima na wamekuwa wakifanya hivyo katika maeneno mbalimbali katika jiji la Dar es Salaam.

Amesema taasisi yao ya Udugu Social Help Welfare sio ya kidini, lakini wengi wao ni Waislamu, na kwamba wanasaidia watu mbalimbali bila kujali dini zao.

“Sisi tunaitwa Udugu Social Help Welfare, tupo Buguruni Malapa, tuko wakina mama 20, tulianza mwaka 2009, tumekuwa tukisaidia watu wenye mahitaji sehemu nyingi na bado tunaendelea kufanya hivyo,” alisema kioongozi huyo.

“Tumesikia changamoto watoto hawa wanazokutana nazo katika kituo hiki, baada ya watoto kueleza changamoto zao, tunamuomba Mwenyezi Mungu atuwafikishe tuweze kusaidiana”, amesema Hajjat Neema.

Amesema kuwa wametoa msaada kwa watoto hao jumla ya vitu vyenye thamani ya shilingi laki sita na elfu sitini na nane (668,000) msaada uliotoka mifukoni mwao kwa kuchangishana kila mwezi.

Hajjat Neema amewataka Waislamu, hasa kina mama kuwakumbuka wenye uhitaji maalumu kwa kuwasaidia na kuwapa faraja kuwahurumia na kuona wao ni sehemu ya jamii.

“Watoto kama hawa wanahitaji ukaribu wetu, hivyo kushirikina nao ni kuwapa upendo ambao nao kama wanaadamu wanauhitaji sana,” amesema Hajjat Neema.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa taasisi ya kulelea watoto yatima na wenye mazingira hatarishi cha Al-Azam Orphanage Center Sheikh Musa Chele ametoa wito kwa wafadhili kuacha kuwatumia watu wa kati kufikisha sadaka zao katika makao ya watoto yatima.

Amesema, kwa muda mrefu watu hao wa kati (Agent) wamekuwa wakitumia fursa hiyo vibaya kwa kujinufaisha wao wenyewe badala ya watoto yatima.

Akielezea historia ya kituo chao, Sheikh Musa alisema Kituo chao kimeanzishwa mwaka 2009 kikiwa na watoto 10, wavulana 5 na wasichana 5, hadi kufika mwaka 2021, walikuwa na watoto 60, kati yao wanawake 35 na wanaume 25.

45 kati ya watoto hao 60, wanaishi katika Kituo na wengine wanalelewa wakiwa majumbani mwao.

Amesema Kituo kinakabiliwa na changamoto nyingi, lakini kubwa ni huduma za afya, watoto wengi hawana bima za afya ili kuwasaidia kupata matibabu bila hofu.

Pia amesema kuna changamoto ya rasilimali fedha za kulipa pango la nyumba, ada za wanafunzi, na chakula, kwa mwezi wanalipa shilingi 300,000 fedha ambazo ni nyingi kwa uwezo wao.

Upande wa mafanikio amesema, Kituo kimeweza kununua kiwanja na kuwaomba wadau kuwajengea nyumba ili watoto wakaishi huko na kuepukana na adha ya kupanga.

 

Latest News

Most Read