Khidmat watoa zawadi ya tiketi ya Umra

 Na Bint Ally Ahmed

Taasisi ya AN-NAHL TRUST imetoa zawadi kwa wanafunzi 175 wa kidato cha nne ambao walifaulu vizuri katika mitihani yao taifa mwaka jana.

Mwanafunzi Hassan Hamid Ussi kutoka shule ya sekondari Lumumba Zanzibar, ambaye ni miongoni mwa wanafunzi hao waliofanya vyema pamoja na kupata zawadi nyingine, alizawadiwa tiketi ya kwenda na kurudi kufanya ibada ya Umra Makka mwaka huu.

“Niseme tu hapa kwamba vijana msitumie mitandao vibaya…ongezeni ujuzi (skills). Kwa mfano wewe ni mhasibu usibweteke na hapo utakapofikia, ongeza mambo mengine yatakayokufanya uwe tofauti na wengine. Waajiri siku hizi wanataka watu wenye kuisadia kampuni na sio mtu mzigo” Alibainisha Bw. Mtambalike.

Mkurugenzi huyo ambaye pia ni miongoni mwa vijana 50 bora wenye ushawishi Tanzania, aliwachukua vijana watatu waliofanya vizuri zaidi katika vijana hao 175, na kuwa sehemu ya watakaokuwa wanapata ujuzi katika kampuni yake ya Sahara Ventures.