Ni walio Magerezani kwa tuhuma za ugaidi

Na Bakari Mwakangwale

MASHEIKH na Waislamu waliopo Magerezani kwa tuhuma za ugaidi, wameomba kukumbukwa kwa Dua kila mara kwani Dua ndio njia sahihi ya kuwasaidia.

Salamu hizo zimefikishwa na Ustadh Ibrahim Mkondo, akiongea na Waislamu katika Dua ya kuwaombea Waislamu hao, iliyosomwa Ijumaa ya wiki iliyopita, katika Msikiti wa Ijumaa, Gongo la Mboto, Jijini Dar es Salaam.

Ustadh Mkondo, alisema viongozi wa Shura kila wanapo watembelea Waislamu hao katika magereza mbalimbali kwa nyakati tofauti, ombi lao kubwa ni kuwaomba kufikisha salaam kwa ndugu zao Waislamu kuwaombea Dua.

Ustadh Mkondo, alisema pia akawataka Waislamu kutenga muda na kwenda kuwatembelea na kuwajulia hali na kile wanachoweza kuwasaidia pia wawasaidie kwani ni haki yao ili kuwapunguzia makali ya maisha ya gerezani.

Alisema, ifahamike kuwa huko magerezani wapo Waislamu wanawake ambao nao wana tuhuma za ugaidi, kwa maana hao ni dada na mama zao ambao nao wanataabika humo magerezani.

Alisema, wanawake hao walikamatwa na kuacha watoto wadogo majumbani mwao, nao kwa sasa wanateseka magerezani kwa miaka kadhaa na haijulikani ni lini watatoka au kuhukumiwa.

Ustadh Mkondo, akawataka Waislamu kuguswa na hali ya wenzao walioko mahabusu kwa tuhuma za ugaidi na wala wasidhani kuwa wao ni wahalifu.

Latest News

Most Read

  • Week

  • Month

  • All