Makanisa 2 yafanya Ihsani

SHULE ya Sekondari ya Kiislamu ya Soni, iliyopo Halimashauri ya Bumbuli Mkoani Tanga, imefanikiwa kuyatwaa Makanisa mawili na kuyageuza kuwa mabweni.

Na Bakari Mwakangwale

Akiongea na Gazeti la An nuur, Mhasibu wa Shule hiyo (Soni Islamic) Bw. Omari Mchengwa, amesema wamefanikiwa kumiliki ardhi iliyojengwa Makanisa hayo baada ya maongezi ya kina baina ya uongozi wa Shule na Viongozi wa Makanisa hayo.

Bw. Mchengwa alisema jumla ya Shilingi Milioni Arobaini zimetumika kuwahamisha wamiliki wa Makanisa yote mawili, lakini akasema ukijumlisha na gharama za michakato ya awali katika kuliendea suala hilo imewaghalimu Shilingi Milioni Hamsini.

Alisema, pesa hizo zimetolewa na mamlaka ya Shule, ambayo ndio iliyofanya michakato yote hadi kufikia muafaka na makubaliano hayo ya kimaendeleo kwa amani na utulivu.

Bw. Mchengwa alisema uongozi wa Shule ulilazikima kuingia katika mazungumzo na Makanisha hayo baada ya kuona mwenendo na uenedesha wa ibada wa ndugu zao hao unawaathiri katika ufundishaji vijana wao.

“Sisi kama Shule ndio tulikuwa waathirika wakubwa kwa uwepo wa Makanisa yale katika taratibu zao za kiibada hali ambayo ilikuwa inaondoa utulivu kwa wanafunzi wetu na hiyo ikawa ni kama changa moto kwetu.” Amesema Bw. Mchengwa.

Awali Bw. Mchengwa alisema katika eneo ilipo Shule walipakana na Makanisa mawili moja likiwa ni la dhehebu la Wapentekoste na lingine la Wasabato, hali iliyopelekea kuwa katika changamoto wakati wa ibada zao, hasa kwaya.

Alisema, baada ya wenzao hao kuafiki kuwaachia maeneo yao ambayo tayari walikuwa wamejenga makanisa na kuendesha ibada zao, sasa Makanisa hayo wameyafanya kuwa ni mabweni.

Bw. Machengwa, alisema lililokuwa Kanisa la Wasabato tokea mwaka jana linatumika kama Bweni la Wasichana baada ya kulikarabati kwa kuweka miundo mbinu ya kibweni kutoka mazingira ya kiibada na Kanisa la Wapentekoste linatumika kama Bweni la wavulana.

Waumini wa Makanisha hayo wamehamishiwa upande wa pili wa barabara itokayo Mombo kwenda Lushoto, kupitia Soni, ambapo kwa sasa wapo umbali wa mita mia tatu kutoka ilipo Shule hiyo.

Akifafanua juu ya makubaliano yao Bw. Mchengwa, alisema kwa Kanisa la Pentekoste walihitaji kufidiwa jengo (Kanisa) ambapo iliwagharimu kiasi cha Shilingi Milioni 15 na Laki Nane kusimamisha jengo hilo na kwamba walikubaliana watoe fidia ya eneo kutokana na eneo walilopelekwa kuwa finyu ukilinganisha na eneo walilowaachia hivyo waliwafidia fidia Shilingi Milioni Tatu.

Ama kwa uopande wa Wasabato walikubaliana kuwajengea jengo la Shilingi Milioni 18 na laki tatu katika eneo walilowanunulia kwa ujumla akasema makubaliano yalikamilika ndipo na wao waliwa kabidhi majengo yao.

Alisema, kihistoria Shule ndio ilianza kujengwa katika maeneo hayo na kwamba kwa kuwa maeneo hayo yalikuwa ya watu binafsi, hivyo wenye maeneo waliuza bila kujali muingiliano wa kile wateja wao walichokusudia katoka matumizi ya ardhi hiyo.

Shule ya Soni Islamic, ipo chini ya Taasisi ya Waislamu ya Soni Islamic Forum (SIF) Shule hiyo ni zao la umoja wa Misikiti ya Tarafa ya Soni, awali wakiwa na lengo la kufungua Chuo cha Dini.

Lakini wazo hilo lilikuja kubadilika baada ya kuona wana fursa ya kuwa na Sekondari ambapo mwaka 2008, waliingia makubaliano na Taasisi ya Islamic Development Foundation (IDF) ili kuanzisha kituo cha elimu chini ya Mkurugenzi Ustadhi Abubakar Mussa.

Most Read

  • Week

  • Month

  • All