Imam Masjid Mtoro amefariki

IMAMU Mkuu wa Msikiti maarufu nchini Tanzania, Masjid Mtoro, uliopo Kariakoo Jijiji la Dar es Salaam, Sheikh Zubeir Yahaya Mussa Alykassajy, amerejea kwa Mola wake.

Na Bakari Mwakangwale

Mwenyezi Mungu anasema, Wale ambao ukiwasibu msiba husema:

‘Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake yeye hakika tutarejea.”

Hayo ndio maneno yaliyotawala katika vinywa vya Waislamu na wale walioandika kupitia mitandao ya kijamii, kufuatia taarifa za kufariki Dunia kwa Sheikh Zubeir.

Sheikh Zubeir ambaye pia ni mwanachuoni wa Kiislamu na Mudir wa Madrasat Abasiyya ya Jijini Dar es Salaam, ametangulia mbele ya haki jioni ya Jumatatu (Machi 4, 2019) kuamkia Jumanne (5, 2019) wiki hii.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali, walijitokeza sambamba na mamia ya wakaazi wa Jiji la Dar es Salaam na vitongoji vyake kushiriki katika mazishi ya Sheikh Yahya Mussa.

Kwa upande mwingine, Masheikh na Maimamu kutoka Misikiti mbalimbali ya Jijini Dar es Salaam, viongozi wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu, nao walimiminika na kuungana na waumini wa Dini ya Kiislamu katika Msikiti wa Mtoro, ambapo taratibu za maziko zilifanyikia hapo, huku visomo na dua zilianza kusomwa kuanzia majira ya saa nne asubuhi ya Jumanne wiki hii.

Sheikh Zubeir aliswaliwa katika Msikiti wa Mtoro na baada ya swalat Aswir, mamia ya Waislamu walilazimika kufunga mitaa ya Kariakoo, Jijini Dar es Salaam na kusimamisha shughuli kwa muda wakiusindikiza mwili wa Sheikh Zubeir, kwenda kuusitiri katika makaburi ya Kisutu, Jijini Dar es Salaam.

Sheikh Zubeir amejipambanua kuwa alikuwa ni mmoja wa Masheikh maarufu Jijini Dar es Salaam na kipenzi cha Waislamu akiwa Imamu wa muda mrefu wa Msikiti huo maarufu wa Mtoro, kutokana na mamia ya Waislamu waliojitokeza kuusindikiza mwili wake.

Katika uhai wake, Sheikh Zubeir amekuwa akiendesha darsa katika Msikiti wa Mtoro na maeneo mengine ya Jiji la Dar es Salaam, huku akijiweka karibu na jamii akiwa na ushirikiano wa karibu na Masheikh na Taasisi mbalimbali za Kiislamu.

Mbali ya Uimamu, Sheikh Zubeir katika uhai wake amesomesha vijana wengi katika Madrasa ya Abbasiyya, huku akiitumikia dini ya Mwenyezi Mungu kupitia Misikiti mbalimbali ya Jijini Dar es Salaam.

Sheikh Zuberi alizaliwa mwaka 1955, Kijijini Kisiju Longoni, Mavunja, Mkoa wa Pwani.

Manamo Mwaka 1962, akiwa na umri wa miaka 7 tu, mjomba wake Mzee Ally Mohamed, alimleta Jijini Dar es Salaam na kumkabidhi kwa Sheikh Ramadhan Abbasi, kwa malezi na Elimu ya Dini.

Sheikh Zuberi alidumu na Sheikh wake akisoma na baada ya kuiva, alikuwa mwalimu katika Madrasa ya Sheikh Ramadhan Abbasi, iitwayo Almadrasatul Abbasiyyah, iliyopo mtaa wa Mkunguni Nyumba Namba 4 Kariakoo.

Miaka ya Sabini Tanzania, ilimpokea Sheikh mwenye asili ya Sudan, Sheikh Abbas Mustafa Maqboul, ambaye kwa kushirikiana na Bakwata, aliasisi kituo cha Elimu Markaz Al-haramain, ambayo iliendesha masomo ya Dini katika majengo ya Shule ya Kinondoni Muslim na jengo la Bakwata (Anjuman) liliopo Mtaa wa Bibi Titi, Mnazi Mmoja, Dar es Salaam, ambapo vijana waliofaulu mitihani ya mwisho walipata fursa ya kuendelea na masomo nchini Saudi Arabia.

Katika mpango huo, Sheikh Zuberi, alikuwa ni mmoja wa vijana waliojiunga na Kituo cha Al-haranain na mwaka 1980, alipata fursa ya kwenda kusoma Elimu ya juu ya Dini katika Chuo Kikuu cha Kiislamu, kilichopo katika mji wa Madinati Al-Munawwarah, Saudi Arabia.

Sheikh Zuberi alirejea nchini mwaka 1987 na kuendelea kufundisha katika Madrasatul Abbaasiyyah na baadae aliteuliwa kuwa Imam wa Msikiti wa Mtoro, Jijini Dar es Salaam.

Sheikh Zuberi alishiriki katika shughuli za Da’awa na huduma za kijamii akiwa karibu na marehemu Sheikh Aboud Jumbe Mwinyi.

Mpaka anafariki, Sheikh Zuberi alikuwa kiongozi wa kundi la Misikiti ya Kariakoo, Jijini Dar es Salaam, iliyokuwa ikitoa misaada ya kibinaadamu kwa wagonjwa walio katika hospitali ya magonjwa ya Saratani ya Ocean Road.

Sheikh Zuberi, ameacha mjane mmoja. Tunamuomba Allah (s w) amjaalie kauli thaabit na kaburi lake liwe katika viwanja vya watu wema wa Peponi na awape subra wafiwa.

 Amin yaa Rabil A’alamina.

Most Read

  • Week

  • Month

  • All