Mashindano ya Qur’an kwa wanawake kufanyika Oktoba 18

Na Bint Ally Ahmed

Mashindano ya kusoma na kuhifadhi Qur’an kwa wanawake watu wazima yanatarijiwa kufanyika Oktoba 18, 2020 kuanzia saa moja asubuhi hadi saa nane mchana katika ukumbi wa City Garden Jijini Dar es Salaam.

Muaandaji wa mashindano hayo taasisi ya Aisha Sururu Foundation, kupitia Mwenyekiti wake, Bi. Aisha Sururu, amesema maandalizi kwa ajili ya mashindano hayo yanaendelea vizuri na kwamba, wanawake wengi wamejitokeza kuchukua fomu za kushiriki.

Bi. Aisha akizungumza na mwandishi wa habari hizi jijini Dar es Salaam hivi karibuni, amewataka kina mama wa Kiislamu wanaoshiriki katika mashindano hayo, kufanya maandalizi ya kutosha ya  kujiweka tayari kwa ushiriki.

Aidha Bi. Sururu amewataka wanawake wa Kiislamu kufanya juhudi kuingia darasani kuisoma na kuelewa dini yao vizuri, ili wapate kufanya ibada zao kwa usahihi na kwa vitendo kuwa tayari watakuwa wana elimu ya uhakika juu kila jambo la ibada husika.

“Kufanya jambo kwa kuwa na uelewa nalo ni bora na inapendeza zaidi kuliko kufanya kibubusa, twendeni Madrasa kina mama, sisi ndio walezi wakubwa wa familia zetu, tukajifunze dini yenu kwa maslahi yetu na famlia zetu ” alisisitiza Bi. Sururu.

 

Latest News

Most Read

  • Week

  • Month

  • All