Ni baada ya kushinda shindano la Qur’an.

Na Bint Ally Ahmed

Bi. Kioni Khatib Sharif, ameibuka mshindi wa kwanza ngazi ya Juzuu 18, na kuzawadiwa zawadi wa kiwanja kufuatia mashindano ya kusoma na kuhifadhi Qur’an kwa akina mama yaliyofanyika jijini Dar hivi karibuni.

Mshindi huyo wa kwanza pia alikabidhiwa pesa taslim shilingi laki tano.

Katika mashindano hayo ya kusoma na uhifadhi wa Qur’an kwa kina mama watu wazima yaliyofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya City Garden, Kariakoo jijini hapa mwishoni mwa wiki iliyopita, mshindi wa pili alikuwa ni Maryam Yunus Ibrahi, kutoka Madrsa Umaif ya jijini Dar na wa tatu ni Saada Juma Ahmad, kutoka madrasa Faraja Islamic Foundation.

Mshindi wa pili alikabidhiwa pesa taslim laki nne na cherahani ya kudarizi na mshindi wa tatu akijinyakulia alizawadiwa shilingi laki tatu na cherahani ya kudarizi.

Mashindano hayo yaliandaliwa na Madrasa Ummul-Muuminiina Aisha Foundation (UMAIFA) ya Buguruni Jijini Dar es Salaam, na washiriki walikuwa ni akina mama pekee kuanzia umri wa miaka 25 hadi 72.

Hayo ni mashindano ya sita (9) ya kusoma na kuhifadhi Qur’an kufanyika, ikiwa ni mwendelezo wa Madrasa hiyo kuandaa mashindano hayo kila mwaka.

Akitoa ufafanuzi juu ya mashindano hayo, msimamizi Ust. Samatta, alisema katika mashindani hayo waligawanya washiriki katika makundi kwa kuzingatia umri wao.

Kwa upande wa Juzuu 15 nafasi ya kwanza ilichukuliwa na Halima Khamis Mjaja, nafasi ya pili ikichukuliwa na Tima Othman Ally na nafasi ya tatu ikienda kwa Bi. Aisha Seif Khamis.

Ust. Samata alisema kulikuwa na kundi ‘A’ lililokuwa la washiriki kuanzia umri wa miaka 25 hadi 44 na kundi ‘B’ ni washiriki kuanzia umri wa miaka 45 nakuendelea.

Kwa upande wa Juzuu tatu mshindi wa kwanza alikuwa ni Bi. Rabia Hassan Kigumi, mshindi wa pili Bi. Zume Hamad Muhunzi na nafasi ya tatu ilichukuliwa na Bi. Salama Khalfan Kisama.

Washindi wa Juzuu ya kwanza kundi A nafasi ya kwanza ilichukuliwa na Maryam Ally Sheha, nafasi ya pili ikaenda kwa Amina Rashid Hasan na nafasi ya tatu ilichukuliwa na Maryam Swaleh Husein.

Juzuu tatu A mshindi wa kwanza alikuwa ni Amina Qasim FAki, nafasi ya pili ikashikwa na Hafwa Omary Shabani na nafasi ya tatu ikatwaliwa na Aisha Abdulrahman Nkoba.

Juzuu tato nafasi ya kwanza ikichukuliwa na Salma Mohamed Iddi, mshindi wa nafasi ya pili alikuwa ni Zuhura Ahmad Bakar na nafasi ya tatu ikaenda kwa Aisha Rajab Dunda.

Juzuu saba nafasi ya kwanza ilichukuliwa na Subra Othmani Ame, nafasi ya pili ikichukuliwa na Rukia Ahmad Bakar na nafasi ya tatu ikaenda kwa Maryam Samueli Simone.

Kwa upande wa Juzuu 10 mshindi wa kwanza alikuwa Aisha Ahmad Ame, nafasi ya pili ilikuwa Aisha Shela Rashid na nafasi ya tatu ikachuliwa na Aisha Ally Omar.

Washindi wote walikabidhiwa zawadi mbali mbali na pesa taslimu.

Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano hayo Ustadh Mohamed Omar Samatta, alisema kuwa Madrasa hiyo ilianzishwa mwaka 1990 na ina jumla ya  wanafunzi  123  kutoka sehemu mbalimbali za jiji la Dar.

Alisema wanafunzi wa Madrassa hiyo wanasoma pia masoma mengine kama vile Masomo ya Qur`an, Tahfeedh, Figh, Sira, Hadith na Tawheed.

Hata hivyo Ust. Samatta, aliwataka akina mama kujiunga na Madrasa mbalimbali ili kuweza kuijua dini yao, lakini pia aliwaomba wasikate tamaa kutokana na kukabiliwa na majukumu mengi ya nyumbani wakaiacha Qur’an.

Aliwasihi kuendelea kujitahidi kutenga muda wao mchache kwa ajili ya kupata elimu hii muhimu ya dini na maisha kwa ujumla, kwani kuikosa elimu hiyo kutawafanya watoke nje ya malengo ya kuumbwa kwao, kwani Qur`an ndio  muongozo wa maisha ya Waislamu wote.  

“Ishikeni Qur`an nawe itakushika siku ya kiama kwani mkifanya hivyo mtazilea nafsi zenu na familia zenu katika misingi ya Qur’an na tutaleta ustawi wa jamii wenye  nidhamu na hofu ya Allah” Alisisitiza Ust. Samatta.

Kauli mbiu ya mashindano ya mwaka huu ilikuwa ni “Qur`an ni mkumbozi wa wanawake” .

 

Latest News

Most Read