Adaiwa Kukiri kuchoma Moto Mtambani

Na Bint Ally Ahmed

Taarifa za Kipolisi zinadaiwa kusema kuwa mtu mmoja anashikiliwa na jeshi hilo baada ya kukiri kuhusika kuchoma moto Shule ya Kiislamu ya Sekondari Mivumoni.

Mtu huyo ambaye anashikiliwa na Polisi, anadaiwa kukiri kuhusika na tukio la pili la kuungua shule hiyo, lililotokea Agosti 8 mwaka huu.

Wakati huo huo, watu wengine 12 wanahojiwa na Polisi kwa tuhuma za kuchoma moto Shule ya Sekondari ya Kiislamu Mivumoni iliyopo Kinondoni jijini Dar es Salaam, likiwa ni tukio la tatu mfululizo ndani ya miezi miwili.

Kamanda wa Polisi Kinondoni jijini Dar es Salaam, SACP Edward Bukombe, amethibitisha kukamatwa na kushikiliwa watu hao kwa mahojiano zaidi, ili kubaini chanzo cha moto huo.

 Kwa upande wake Katibu wa Msikiti wa Mtambani unaomiliki shule hiyo, Sheikh Abdallah Ally, amesema mtuhumiwa anayehusishwa na tukio la siku za nyuma la kuungua shule hiyo ameshafikishwa mahakamani.

Hata hivyo alisema uchunguzi wa matukio ya siku za nyuma na hili la karibuni Agosti 31 wamewaachia polisi waendelee na uchunguzi wao na watakapokamilisha watapewa ripoti.

“Kuna mtu moja anasadikiwa kukiri kuhusika na kuchoma moto shule yetu, huyu alishakamatwa na yupo chini ya Polisi hadi muda huu, lakini watu wengine 12 waliokamatwa katika tukio la hivi sasa bado mahojiano na uchunguzi zaidi wa Polisi unaendelea,” alisema Sheikh Abdallah Ally.

Sheikh Ally amesema kuwa tukio la kuungua moto mara kwa mara shuleni hapo limewafedhehesha sana na kuwatia simanzi, lakini bado haijajulikana kuna nini hasa ambapo hii ni mara ya tatu ndani ya muda mfupi shule inaungua, huku kukiwa hakujapatikana taarifa yoyote juu ya moto huo na sababu yake.

Katika tukio la shule kuungua moto Agosti 31, ilielezwa kuwa moto huo ulianzia katika ofisi ya Mwalimu Mkuu na kuenea katika mabweni mawili ya wanafunzi yenye vitanda 102, magodoro na kisha kufika katika ofisi nyingine nne ikiwemo ya matron.

Kwa kushirikiana na Jeshi la Zima Moto, moto huo ulidhitiwa na kinachoendelea kwa sasa ni upelelezi ili kubaini nini hasa kinachosababisha moto huo kujirudia mara kwa mara shuleni hapo.

Ofisi na mabweni ya Shule ya Sekondari ya Mivumoni Islamic iliyopo katika Msikiti wa Mtambani wilaya ya Kinondoni Jijini Dar es salaam, yalimeungua moto alfajiri ya Agosti 31, 2020.

Inaelezwa  kuwa hii ni mara ya tatu  kwa shule hiyo kuungua  ndani ya miezi miwili, ambapo ajali ya kwanza ilitokea  Julai, 17 likifuata  tuko la Agosti 4 na sasa Agosti 31 imetoka ajali ya tatu katika shule hiyo hiyo.

Moto huo ulitokea wakati waumini wakijiandaa na swala ya Alfajir.

Wanafunzi hawakuwepo mabwenini wakati ajali hiyo kwa kuwa katika tukio la awali la Agost 8, uongozi wa shule uliwarudisha wanafunzi hao wa bweni majumbani kwa muda, wakati uongozi wakitafuta ufumbuzi wa janga hilo kabla ya kuwarejesha.

Imamu wa Msikiti wa Mtambani, Imam Suleiman ameiomba Serikali kuisaidia shule hiyo kujua chanzo cha moto huo unaojirudia kila mara na kwa kipindi kifupi.

Aidha Imam Suleiman  amewataka Waislam kuwa na subra wanapopatwa na mitihani kama hii, kwa kuwa Allah (sw) amewataka kusubiri na kuzidisha dua kwani Waislamu kimbilio lao wanapokutana na mitihani mizito, huwa kilio chao wanakipeleka kwa Mola wao aliyetukuka.

Pia amewaomba Waislam kutoa msaada wao wa hali na mali kusaidia kurejesha miundo mbinu ya shule hiyo katika hali ya kawaida, ili wanafunzi waendelee na masomo yao kwani wapo wanaojiandaa na mitihani ya taifa  kwa kipindi hiki.

Amewataka Waislam kushikamana na kuzidisha umoja na upendo hasa katika kuwapa moyo na kuwatia nguvu uongozi, wanafunzi na waumini wa Mtambani, kwani wapo katika kipindi kigumu sana, ambacho hawajui nini hatma ya majanga hayo yanayoendelea kujitokeza kila mara.Moja wa mashuhuda wa atukio hilo jina lake halikupatikana amewaasa viongozi wa taasisi za Kiislamu na Waislamu kwa ujumla kuangalia mifumo ya umeme katika taasisi zao, huku akiwashauri kuwa na vifaa maalumu vya kugundua hali ya hatari inapoanza kujitokeza katika majengo yao.

Aidha wametakiwa kuimarisha ulinzi katika shule na vyuo ikiwemo kuweka kamera, ili kuonyesha mienendo ya watu wanaoingia na kutoka katika sehemu hizo.

Imamu Suleiman amewaomba Waislamu kote nchini kuwachangia chochote walicho nacho kupitia namba hii ya simu 0713 098 959 au unaweza kufika shuleni hapo, ili kuirejesha shule katika hali ya kawaida na wanafunzi waendelee na masomo yao.

Alisema wanalazimika kuomba msaada kwa kuwa hali ya miundo mbinu shuleni hapo imeharibika sana, ikiwemo magodoro, vitabu na mahitaji yote ya muhimu.

Latest News

Most Read