Mataifa Ulaya yatakiwa kuacha kuona Uislamu kama tishio

Mkurugenzi katika kitengo kinachohusika na mawasiliano Ikulu ya rais mjini Ankara, Fahrettin Altun, ametolea wito kwa mataifa ya Ulaya kuacha kuona Uislamu kama tishio.

MKurugenzi huyo amewataka viongozi katika sekta tofauti ndani ya mataifa ya Ulaya kuacha kuchukulia Uislamu kama tishio katika mataifa yao.

Alisema jambo ambalo linahitajika katika jamii ni usawa bila ya kujali tofauti zilizopo katika imani na mitazamo katika masuala tofauti.

Ripoti iliyotolewa na kitengo kinachohusika na taasisi ya SETA, imeonyesha kuwa chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu Ulaya imezidi kuongezeka  mwaka 2019.

Katika hotuba yake aliyotoa katika ufunguzi wa Baraza kwa njia ya video, Fahrettin Altun alisema kwamba Uislamu sio tatizo barani Ulaya.

Kwa mujibu wa Altun, Uislamu sio tishio kwa kuwa kila kukicha, taarifa zinaripoti vitendo vya mauaji na uhalifu dhidi ya binadamu katika mataifa tofauti, unyanyasaji nchini Marekani, nchini India Waislamu wanashambuliwa hadi kuuawa na Wahindu wenye itikadi kali za kidini bila ya kukemewa na yeyote yule.

Mkurugenzi huyo katika Idara hiyo ya mawasiliano Ikulu pia alikemea kitendo cha kupewa tuzo ya Nobel ya amani huko Myanmar, kwa mtu ambaye anafahamika vyema kuhusika na mauaji ya Waislamu wa jamii ya Rohingya.trt.net.tr

Latest News

Most Read