Na Andre Vltchek

Januari 25, 2019 - Mtandao wa Kupashana Habari

NI mpya na siyo mpya, lakini ina uovu mbaya na wa kutisha - aina mpya ya kupindua serikali Marekani iliyotengeneza, na sasa inatumiwa dhidi ya Venezuela.

Bila shaka mapinduzi ya kijeshi na majaribio ya mapinduzi kama hayo, yanaweza kuitwa kuwa ni mambo ambayo nchi za Magharibi zimezoea kufanya na yametumiwa na Marekani, Uingereza na nchi nyingine za kibeberu dhidi ya nchi nyingi tu zenye taabu nyingi katika mabara yote.

Katika bara la Amerika ya Kusini, kimsingi kila nchi imekuwa mhanga wa mapinduzi ya kijeshi. Huko Asia, kutoka Indonesia hadi Thailand, na Mashariki ya Kati, kutoka Iran hadi Misri na Syria. Wakati wowote ambako watu wa nchi fulani walidiriki kuwapigia kura kuingia madarakani wafuasi wa siasa za ujamaa, ukomunisti, upinga ukoloni au wengine waaminifu tu waliotaka kuwatumikia watu wao, nchi za Magharibi zimeingilia kati kwa rushwa, na kuingiza wasaka tonge ndani ya utawala na jeshi, wakapandua serikali zilizochaguliwa au za kimapinduzi na kuweka madarakani serikali katili tiifu kwa maslahi yao. Maelfu walikufa, mara nyingine mamilioni, lakini Himaya (ya Marekani) haikujali kitu, mradi inachotaka ndicho kinafuatwa.

Kumekuwa na miririko bayana wa jinsi nchi za Magharibi zilivyounda vitendo vyake ya ugaidi dhidi ya takriban nchi zote zinazopenda uhuru duniani. Lakini kile ambacho nchi za Magharibi sasa zinafanya kwa Venezuela, ni kitu kingine, na cha kuvuka kabisa mpaka. Vitendo vya uadui dhidi ya Rais Nicholas Maduro na marafiki zake, havina kabisa chembe ya kujali au kufanya vitu kwa tahadhari kama ilivyokuwa awali. Walitaka kudhihirisha kwa njia ya kikatili nani mtawala halisi wa dunia, na ni nani ameshika usukani. Hii 'demokraia ya nchi za Magharibi' ikiwa katika haiba yake halisi!

Wakati uliopita, Marekani ilijaribu kumpindua Hugo Chavez; ilijaribu kuikatia chakula Venezuela, kufanya mfumo wake wa tiba ufyatuke, halafu kumwua Maduro. Ilifikia uhaba wa vyakula, hata karatasi za msalani. Iliwaelekeza 'vijibwa mpakato' kutukana mapinduzi ya ki-fikra za Simon Bolivar, mkombozi wa jadi wa bara hilo.

Sasa katika tukio la hivi karibuni, utawala wa Marekani umemteua mhaini wake unaompenda zaidi katika Jamhuri ya Kijamaa ya Venezuela, kada mhaini aitwaye Juan Guaido, ambaye kwa muda mfupi alikuwa Spika wa Bunge la Venezuela, 'ukimtambua' kuwa 'Rais wa Muda' wa nchi hiyo.

Bila shaka, kabla Guaido kwanza kujitangaza, kwa maringo, Rais wa Venezuela, mara moja alikumbushwa na Mahakama Kuu ya Rufani ya nchi hiyo, ambayo ilimkataa kama Spika (mwenyekiti) wa Bunge. Hivyo labda tuseme mwenyekiti wa Bunge aliyepita.

Lakini kampeni ya propaganda ya nchi za Magharibi ikapamba moto, na kufumba na kufumbua ikawa haina tena vizuizi. Matokeo yake ni kuwa sasa haiwezekani kusoma chochote kuhusu uamuzi wa Mahakama Kuu ya Rufani labda mtu atafute vyombo vya habari ambavyo si vya Magharibi.

Hivyo tuende 'huko.' Kama ilivyoripotiwa na shirika la habari la Iran, Tasnim, Januari 22, 2019:

"Jaji Mkuu wa Mahakama Kuu ya Rufani ya Venezuela Maikel Moreno alitangaza Jumatatu kuwa majaji wamemkataa Juan Guaido kama kiongozi wa Bunge linaloshikiliwa na upinzani."

Na shirika la Russia, RT, siku moja kabla lilisema:

"Mahakama Kuu ya Rufani ya Venezuela imetangaza kuwa vitendo vyote vya Bunge la nchi hiyo havina uhalali wa kisheria, baada ya Bunge hilo linaloshikiliwa na upinzani kutangaza kuwa kuchaguliwa kwa Rais Nicholas Maduro kuwa siyo halali."

Pia, Waziri wa Mambo ya Nje wa Venezuela, Jorge Arreaza, alimkaripia Guaido hapo Januari 21, 2019:

"Unamwona mtu huyu, ambaye hakuna mtu anamfahamu Venezuela - unauliza barabarani, 'Nani huyu Juan Guaido?' na hakuna anayemfahamu - lakini anasukumwa kusema kuwa ndiye rais mpya, na Marekani."

Na alisema hivyo! Tarehe 23 Januari, 2019, mbele ya kundi la mashabiki wake jijini Caracas.

Halafu, siku moja baadaye Rais Donald Trump 'alimtambua' kama rais wa muda wa nchi hiyo. Canada ilifanya hivyo pia. Kama ilivyofanya Ufaransa, hivi sasa ikiwa ni beberu wa ngazi ya pili aliyepania kurudisha nafasi yake kama dola ya ukoloni-mamboleo. Ilifuatiwa na kikaragosi cha Marekani, Umoja wa Nchi za Amerika ya Kusini (OAS), ikiwa na nchi za kifashisti kama Brazil na Colombia ambao sasa ndiyo wako mstari wa mbele.

Leo hivi, dunia imegawanyika wasiwazi, wakati China, Russia, Iran, Uturuki, Syria, Afrika Kusini, Bolivia, Cuba, Mexico, Uruguay na nchi nyingine nyingi zikiwa thabiti nyuma ya serikali halali ya kimapinduzi ya Rais Maduro.

Mpambano hauwezi kuepukika. Venezuela iliwatimua maofisa wote wa kibalozi wa Marekani na kukatisha mahusiano yote na Marekani. Marekani ilikataa kuwaondoa maofisa wake wa ubalozi kutoka Caracas, ikitangaza kuwa serikali ya Venezuela 'haina uhalali.'

Hii inakaribia kabisa na kutangaza vita. Marekani inakataa kuutambua uhuru wa Venezuela. Inakuwa na haki ya kuwachagulia watu wa Venezuela nani rais wao halisi! Inatambua tu umiliki wake usiopingika juu ya ukanda wote wa mabara ya Marekani na sayari kwa jumla, ikidharau sheria ya kimataifa.

Ni utoto, kujiona, haikubaliki na kuota ndoto mchana. Lakini inatokea katika hali halisi. Na kama haitasitishwa, hapo Caracas, njia hii mpya ya 'kueneza mapinduzi ya dola,' na kukazia udikteta wa dunia nzima, unaweza kuenea katika maeneo mengine duniani.

Licha ya kuwa kuna vipengere vipya vinavyojitokeza, hali hiyo kwa kiwango kikubwa inafanana na ile ya Syria. kama ilivyoelezwa kwa TASS (Shirila la Habari la Russia) hapo Janujary 24, 2019, na Balozi wa Venezuela nchini Russia, Carlos Rafael Faria Tortosa.

Utawala wa Venezuela unajua kuwa Marekani inataka kufanya hali iwe kama Syria, kuwa na 'serikali iliyo\ uhamishoni' hapo Caracas. Baada ya Makamu wa Rais wa Marekani Mike Pence alitoa rai ya kupinduliwa kwa serikali hiyo, rais wetu aliamua kuvunja uhusiano wa kibalozi na utawala wa Marekani na kuwataka maofisa wa ubalozi wa Marekani kuondoka ndani ya saa 72. Hili ni jibu la kutosha ambalo rais wetu jasiri alitoa kwa uingiliaji kati huo usio na kificho. Hakuna nchi inayoruhusu nchi nyigine kutoa maoni kuhusu mambo ya ndani ya nchi nyingine, hasa pale inapokuwa ni suala la kuondolewa (kwa utawala uliopo).

"Tunajua hatua zinazofuata ni zipi. Marekani sasa itakuwa na kitu cha kuhalalisha (vitendo vyao) kuwa kuna serikali mbili nchini humo kama walivyofanya kwa rafiki yetu mkubwa Syria, na Rais Bashir el Assad na watu wake. Waliunda serikali iliyoko nje ya nchi, kitu kichosababisha uharibifu mkubwa, maisha ya watu wengi kupotea na kuharibiwa kwa miundombinu nchini humo.

Hivi Venezuela itaomba msaada wa moja kwa moja kutoka Russia, kama Syria ilivyofanya miaka mingi iliyopita, huku ikipigania kuishi? Bado hakuna uhakika licha ya kuwa uwezekano huo upo. Venezuela inatazamia kupata msaada wa ziada kutoka Russia, Iran, China, Cuba na nchi nyingine za kijamaa au zilizo huru (na ubeberu wa Marekani).

Kwa Venezuela, njia pekee ya kuishi ni kukata utegemezi wote kwa nchi za Magharibi mara moja. Marekani inaitishia Venezuela na kuwekewa vikwazo vingine na hata kuzuiwa kuuza mafuta nje.

Hakuna sababu ya kukata tamaa. Lakini serikali ya Maduro inabidi kwa haraka ijiondoe katika mahusiano yaliyopo. Kuna nchi nyingi ambazo sehemu ya ukanda wa NATO ambazo ziko tayari kununua mafuta ya Venezuela, na pia kwa uwiano wa faida kuwekeza katika miundombinu yake na viwanda. Russia, Iran, China na Uturuki ndizo muhimu zaidi lakini ziko nyingine nyingi.

Lazima kuwa na mkakati mpya wa jinsi ya kuondoa maumivu ya raia wa kawaida wa Venezuela. Hili pia lazima lianzie nje ya umiliki wa nchi za Magharibi, hata nje ya Amerika ya Kusini, bara linalofahamika kwa dola za kikatili zinazotokana na walowezi wanaotokea Ulaya. Ni kutokuwepo mshikamano kabisa kihistoria, ujasiri na kukubali utawala wa nchi za Magharibi. Shujaa mkubwa zaidi wa miaka ya karibuni barani humo, Hugo Chavez, alikufa akijaribu kujenga Amerika ya Kusini yenye umoja, inayojiamini, na ya kijamaa. Ila akapigwa kisu cha mgongoni na kutemewa mate na mengi kati ya mataifa matiifu kwa utumwa katika bara hilo. Cuba iliachwa kabisa baada ya kuangamia kwa iliyokuwa Urusi ya kijamaa, ikabidi iokolewe na China.

Nchi hiyo lazima ijikusanye. Inabidi ipambane. Ipiganie kuishi. Washirika wake wakiwa wameungana, wakiwa tayari kuilinda Venezuela, kama jinsi ilivyotokea Syria.

Venezuela inapata taabu na kupambana kwa ajili ya binadamu, siyo kwa ajili yake peke yake. Ikiwa na jina la Chavez na Ujamaa mdomoni mwake.

Russia imesimama pamoja na mshirika wake, Venezuela. Hapo Januari 24, Shirika la Habari la Sputnik liliandika:

Russia inaionya Marekani dhidi ya kuingilia kijeshi katika mambo ya Venezuela, itakuwa ni janga; Naibu Waziri wa Mambo ya Nje Sergei Ryabkov alisema.

"Kama tunavyoona hali ya Venezuela inavyojengeka, tunaona utayari wa kundi fulani la nchi, ikiwa pamoja na Marekani, kutumia majukwaa tofauti kama Umoja wa Nchi za Amerika, kuongoza shinikizo kwa mshirika wetu Venezuela chini ya visingizio tofauti. Lakini tumeunga mkono kuiunga mkono Venezuela ambayo ni mshirika watu kimkakati." Kwa nchi iliyoharibiwa na kampeni kama hiyo ya kuharibu umoja wa nchi na uthabiti wa dola kama inavyotokea Venezuela, Shirika la Habari rasmi la Syria, SANA lilikuwa na ujumbe wa kuunga mkono serikali halali ya Venezuela.

"Jamhuri ya Kiarabu ya Syria inalaani wa ukali wote unaowezekana kuvuka mipaka kwa Marekani na uingiliaji wake wa wazi katika mambo ya Jamhuri ya Kibolivari ya Venezuela, jambo ambalo linavunja kanuni zote za kimataifa na sheria na shambulio lisilo la uficho dhidi ya uhuru wa Venezuela," ofisa wa Wizara ya Nje na Waliohama Nchi ilisema.

Ofisa huyo alisema sera za kiharibifu zilizochukuliwa na Marekani katika sehemu tofauti za dunia na kutokujali uhalali wa kimataifa ndiyo sababu kubwa ya misuguano na machafuko katika dunia yetu.

Jamhuri ya Kiarabu ya Syria inarudia kukataa kwake kwa uingiliaji wa wazi wa Marekani, na inathibitisha tena kuwa bega kwa bega na uongozi wa Venezuela na watu katika kulinda uhuru wa nchi na kupangua njama za uadui za utawala wa Marekani.

Katika wakati uliopia, nchi zilikubali vita nchi za Magharibi ilizopeleka dhidi yao kama kitu kisichozuilika. Lakini sasa hali inabadilika. Russia, Cuba na Syria. Iran na China, na sasa Venezuela zinakataa kusalimu amri, na zinakataa kujadili chochote na magaidi (wa Marekani).

Aleppo, ambayo nimeuita ni Stalingard ya Mashariki ya Kati (pambano kuu la vita vya pili vya dunia ambako ufashisti ulishindwa) ulisimama wima, ukapigana, ukazuia na kushinda maadui wakali sana. Sasa Caracas, ambayo ndiyo Leningrad ya Amerika ya Kusini (ambapo mapinduzi yalifaulu mwaka 1917) umezingirwa, unakufa njaa, lakini umepania kupigana dhidi ya uvamizi wa kigeni na makada wahaini.

Duniani kote, watu inabidi wajikusanye na kupigana, kwa kila njia, dhidi ya ufashisti na kwa ajili ya Venezuela.

(Makala hii The Coup in Venezuela Must Be Resisted imeandikwa na Craig Murray na kutafsiriwa kwa Kiswahili na Anil Kija.)

 

Most Read

  • Week

  • Month

  • All