Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) limetahadharisha kuhusu njaa na hali mbaya inayowasumbua raia wa Yemen.

Shirika hilo limetangaza kuwa hali ya raia wa Yemen ni mbaya sana na kwamba, yaweza kusababisha maafa makubwa ya njaa.

Ripoti iliyotolewa na shirika hilo imesema kuwa, baadhi ya misaada ya chakula inayotumwa katika maeneo mbalimbali ya Yemen inaporwa na kuuzwa masokoni.

Ripoti hiyo imeongeza kuwa, Shirika la WFP linafanya jitihada za kujaribu kufikisha misaada ya chakula kwa karibu Wayemeni milioni 12 wanaosumbuliwa na baa la njaa.

Awali Umoja wa Mataifa ulikuwa umetangaza kuwa, kuna uwezekano mkubwa hali ya raia nchini Yemen ikawa mbaya zaidi katika mwaka huu wa 2019 na kutangaza kuwa, hatari ya njaa inaikabili zaidi ya asilimia 75 ya watu wote wa jamii ya nchi hiyo.

Yemen ilivamiwa na kushambuliwa na Saudi Arabia na washirika wake wanaosaidiwa na Marekani, Israel na nchi nyingine za Magharibi mwaka 2015 na inaendelea kuzingirwa baharini, nchi kavu na angani.

Mashambulizi hayo ya Saudia ya washirika wake yameua maelfu ya raia wasio na hatia na kuwalazimisha mamilioni ya wengine kuwa makimbizi.parstoday.

Latest News

Most Read