Waziri Mkuu wa New Zealand, Jacinda Ardern, ameahidi uwajibikaji wa serikali yake kuhusu ripoti ya hujuma dhidi Msikiti mjini Christchurch.

Waziri Mkuu wa New Zealand, Jacinda Ardern, ameahidi uwajibikaji wa serikali yake kuhusu ripoti ya hujuma dhidi Msikiti mjini Christchurch.

Siku ya Jumapili, Ardern alikaa kwa muda wa saa mbili na waathirika pamoja na familia za waliouawa katika hujuma hiyo, kabla ya kuzinduliwa ripoti ya Tume ya Kifalme Kuhusu Mashambulizi Dhidi ya Misikiti Christchurch.

Katika hujuma dhidi ya Misikiti miwili ya Christchurch Machi 15, mwaka jana, gaidi wa Kikristo aliwaua Waislamu 51 waliokuwa katika swala ya Ijumaa.

Mwezi Agosti Mahakama nchini New Zealand ilimhukumu kifungo cha maisha jela Brenton Tarrant, baada ya kupatikana na hatia ya kuwaua Waislamu hao 51.

Hakimu aliyetoa hukumu hiyo alikiri kuwa hiyo si adhabu tosha kwa jinai iliyotendwa na gaidi huyo mwenye itikadi kuwa wazungu ni wanadamu bora zaidi watu wengine wote.

Tarrant, raia wa Australia mwenye umri wa miaka 29, alikiri kutekeleza mauaji ya watu 51 na kujaribu kuwaua wengine 40, na pia amekiri kutekeleza kitendo cha kigaidi katika hujuma ya ufuatuaji risasi kiholela dhidi ya waumini wa Misikiti miwili mjini Christchurch.

Katika shambulizi la kigaidi la Machi 15 2019 katika Misikiti ya Linwood na al-Noor mjini Christchurch, Waislamu 51 waliuawa na wengine karibu 50 kujeruhiwa.

Jaji Cameron Mander wa Mahakama Kuu ya Christchurch, alisema Tarrant hajaonyesha kujuta na hiyo hata akibaki jela umri wake wote, adhabu hiyo haiwezi kutosha kufidia jinai zake.

Aidha alisema katika hukumu hiyo ya maisha gerezani, Tarrant hatakuwa na haki ya kuomba kupunguziwa adhabu. (IQNA).

Latest News

Most Read