ukurasa wake wa Facebook

Ni baada ya kutaka bidhaa za Israel zisusiwe

Shirika la mtandao wa kijamii wa Facebook limeufunga ukurasa wa Jumuiya ya Kimataifa ya Maulamaa wa Kiislamu (IUMS), baada ya jumuiya hiyo kutoa fat’wa yake ya kuwataka Waislamu wasusie bidhaa za utawala wa Kizayuni wa Israel.

Jumuiya hiyo wiki hii ilitoa fat’wa ya kuwajibisha kuwekewa vikwazo vya kila upande utawala wa Kizayuni.

Fatwa hiyo inasema ni haramu kununua na kuuza bidhaa za utawala wa Kizayuni hadi utawala huo utakapoacha kuzikalia kwa mabavu ardhi za Waislamu.

Jumatano wiki iliyopita Jumuiya hiyo ilitangaza kuwa, uongozi wa Facebook umeufunga ukurasa wake baada ya kutoa fat’wa ya kuharamisha kununua na kuuza bidhaa za utawala wa Kizayuni.

Jumuiya hiyo imetoa fat’wa hiyo ili kulinda na kuhami uadilifu katika Uislamu, hususan kadhia ya Palestina na imesisitiza kuwa itaendelea na msimamo wake huo bila ya kutetereka.

Wito huo unakuja wakati ambao mwaka wa 2020, nchi nne za Kiarabu ambazo ni Umoja wa Falme za Kiarabu, Bahrain, Sudan na Morocco zilitangaza kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala wa Israel, hivyo kujiunga na Misri na Jordan ambazo zinautambua utawala huo ghasibu.

Katika miaka ya hivi karibuni, mashirika hayo mengi duniani yanaunga mkono vuguvugu la BDS la kuusussia utawala wa Israel kibiashara, kiuchumi, kiutamaduni na kielimu.

Vuguvugu hilo la kimataifa la Boycott, Divestment and Sanctions (BDS) linawaunga mkono Wapalestina kwa kuendesha kampeni dhidi ya Israel kwa kuisusia, kuitenga na kutoshirikiana nayo katika uwekezaji. (IQNA).

 

 

Latest News

Most Read

  • Week

  • Month

  • All