Shule ya Waislamu mjini New Castle, Uingereza imehujumiwa na watu wenye chuki dhidi ya Uislamu ambao walivunjia heshima nakala za Qur'ani Tukufu katika shule hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa, Akademia ya Bahr mjini Newcastle ilihujumiwa wiki hii Jumatatu jioni ikiwa ni mara ya pili shule hiyo kulengwa katika kipindi cha miezi mitatu.

Mkuu wa shule hiyo, Imam Abdul Muheet, amesema genge lililohujumu shule hiyo na kuvunja madirisha kabla ya kuchana nakala za Qur'ani na kuzitupa sakafuni.

Alisema alipigiwa simu na kufika shuleni hapo kabla ya wahalifu hao kuondoka na aliwasikia wakisema eti Waislamu ni magaidi.

Tukio hilo la Newcastle limekuja siku chache baada ya Misikiti 5 kushambuliwa katika mji wa New Castle nchini Uingereza.

Watu wawili walitiwa mbaroni kufuatia mashambulizi hayo yaliyokuja chini ya wiki moja baada ya gaidi kushambulia Misikiti mjini Christchurch New Zeland na kuwaua shahidi zaidi ya Waislamu 52. (IQNA).

 

Latest News

Most Read