Idara ya Polisi Ireland imewaruhusu maafisa polisi wa kike ambao ni Waislamu kuvaa vazi la staha la Hijabu.

"Ni matumaini yangu kuwa hatua hii itawahimiza raia wa jamii za walio wachache kujiunga na kikosi cha An Garda Síochána (Kikosi cha Polisi cha Jamhuri ya Ireland)," alisema Mkuu wa kikosi hicho, Kamishna Drew Harris.

Aidha alisema Masingasinga nao pia wataruhusiwa kuvaa vilemba kama sare ya polisi.

Katika taarifa rasmi, Idara ya Polisi Ireland imesema hatua hiyo inaendana na maamuzi sawa na hayo yaliyochukuliwa na Idara za Polisi za nchi nyingine za Kimagharibi kama vile Scotland, New Zealand, Uingereza, Australia na Canada.

Aliongeza kuwa, wanalenga kuzihakikishia jamii za wachache nchini humo kuwa Idara ya Polisi ni shirikishi katika ajira na inalipa uzito suala la kuwa na maafisa wa jamii zote.

Kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2016, idadi ya Waislamu nchini Ireland inakadiriwa kuwa 65,000 kati ya watu wote takribani milioni 4.8. (IQNA).

 

 

 

Most Read

  • Week

  • Month

  • All