Morocco imejiondoa katika muungano wa kijeshi unaoongozwa na Saudi Arabia katika vita dhidi ya Yemen.

Afisa mmoja wa serikali ya Morocco ametangaza Alhamisi kuwa nchi yake haitashiriki tena katika uingiliaji kijeshi au vikao vinavyofanyika katika ngazi ya mawaziri katika muungano wa kijeshi unaoongozwa na Saudia dhidi ya taifa la Yemen.

Habari ya kujitoa Morocco katika muungano vamizi wa kijeshi unaoongozwa na Saudia dhidi ya Yemen inatangazwa katika hali ambayo, mnamo tarehe 24 Januari, Waziri wa Mambo ya Nje wa Morocco Nasser Bourita, katika mahojiano na Al Jazeera alisema kuhusu kushiriki nchi yake katika muungano huo na kwamba, hivi karibuni, Morocco haijashiriki katika mazoezi mengi ya kijeshi na vikao vya mawaziri vya muungano wa kijeshi dhidi ya Yemen.

Morocco tayari imeshamuita nyumbani balozi wake aliyekuwa mjini Riyadh, Saudi Arabia kwa ajili ya mashauriano.

Saudia ilianzisha mashambulizi dhidi ya Yemen mwishoni mwa mwezi Machi 2015 kwa lengo la kumrejesha madarakani Abdrabbuh Mansour Hadi, rais wa zamani wa nchi hiyo aliyejiuzulu na kutoroka nchi.

Hata hivyo Saudi Arabia na washirika wake wameshindwa kufikia malengo yao hayo huku wakisababisha maafa makubwa ya kibinadamu ikiwa ni pamoja na kuwaua raia wasiopungua 15,000 wasio na hatia.

Idadi kubwa ya watoto na wanawake ni miongoni mwa waliopoteza maisha katika vita hivyo nchini Yemen, ambapo kwa ujumla wake watu wasiopungua 15,000 wameuliwa katika vita hivyo vinavyoongozwa na Saudia ikishirikiana na washirika wake wa Magharibi hasa Marekani. (IQNA).

 

 

 

Amenukuliwa akisema, "Sasa mimi ni Muislamu.

Taarifa zinasema Van Klaveren, alisilimu na kuukubali Uislamu katika maisha yake mnamo Oktoba 26 mwaka 2018, hatua ambayo iliwashangaza marafiki na maadui wake.

Van Klaveren alijitenga na Wilders mwaka 2014 kutokana na matamshi ya kiongozi huo wa Freedom Party, ambaye aliwachochea Waholanzi wawatimue watu wenye asili ya Morocco.

Van Klaveren aliunda chama kipya alichokiita "For Netherlands” (VNL), lakini alistaafu katika siasa baada ya kushindwa kushinda kiti katika uchaguzi wa mwaka 2017.

Said Bouharrou wa Baraza la Misikiti ya Wamorocco Uholanzi amempongeza Van Klaveren na kusema ni hatua kubwa kwa mtu ambaye alikuwa mpinzani mkubwa wa Uislamu kutambua haki na kuongeza kuwa ni ujasiri pia kwake kutangaza uamuzi wake hadharani. (IQNA).