Na Omar Msangi

Kwa wadadisi wa mambo, watazame taarifa hii katika youtube kabla haijafutwa. Anuwani yake ni:

Riverside Kenya Terror Attack Hoax (BAD ACTING) Sydney SEES.” Angalia pia: Nairobi Terror Attack HOAX (BAD ACTING).

Ukishaitazama na pengine kuirejea kiasi mara mbili tatu hivi, na kujitahidi kuelewa, angalia tena ‘clips’ hizi:

  1. Riverside Terror Attack Nairobi January 15, 2019, it was like a movie.
  2. Kenya Hotel Attack Hoax (Sign of deception):
  3. Just watching about it on BBC youtube.

Ukishazitazama hizo clips tatu, pitia taarifa ya Luke Potter (SAS Soldier), kachero wa kikosi maalum cha Uingereza anayesifiwa kwamba kwa ujasiri wake amesaidia sana uokozi katika tukio hili la kigaidi. Wako wachambuzi wengine ambao baada ya kupitia taarifa zake wametilia shaka kisha wakahitimisha na kuridhika kwa kusema:

 "The Terrorist Attack In Kenya" was a HOAX. They carelessly used the same script as the previous False Flag in Nairobi with an "Off duty SAS guy just happening to be on the scene in time to be the ""HERO"".

Lakini pia wanatilia shaka uwepo wa kachero mwingine akitajwa kwa jina la Inayat Kassam. Kama ilivyokuwa kwenye shambulio la kigaidi Westgate mwaka 2013 akiwa mstari wa mbele katika mashambulizi, huyu bwana anaonekana tena katika shambulio hili, lakini katika hali ya kujiamini mno akiwa na vazi la kawaida tu bila hata ya fulana ya kukinga risasi huku akijitosa tu kunakodaiwa kuwa wapo magaidi. Katika vyombo vya habari vya Kenya hivi sasa Inayat (kama ndio jina lake au ni jina la kazi hatujui), anatajwa kama shujaa.

Sasa tuendelee. Lazar Berman, mwandishi wa habari wa gazeti la The Times of Israel, aliripoti katika gazeti hilo la tarehe 29 Septemba, 2013 kwamba Israel ilikuwa imetoa taarifa kwamba Kenya itashambuliwa na magaidi na kwamba magaidi hao watakuwa ama wa kutoa Iran au wale wa Hezbollah. Na kweli, Kenya ikapigwa katika lile shambulio la Westgate Mall, japo walitajwa Al Shabaab.

Naye mwandishi Jason Burke wa gazeti la The Guardian la Uingereza katika toleo lake la Jumatano 16 Januari, 2019 aliripoti kuwa Kenya ilikuwa imeonywa (na Marekani) kwamba itapigwa na Al Shabaab. Na kweli, siku ya Jumanne Januari 15, 2019, Kenya ikapigwa.

Ilikuwa ni siku ya Jumanne majira ya alasiri ambapo zilianza kutolewa habari kwamba limetokea shambulio la kigaidi jijini Nairobi. Taarifa za awali zilidai kuwa, kulikuwa kumesikika mlipuko mkubwa na milio ya risasi katika hoteli ya kifahari ya Dusit (Westlands district) na kwamba watu kadhaa walikuwa wameuliwa.

Kutoka jioni hiyo mpaka usiku, vyombo vya habari vya Kenya na vile vya nje, vikawa na ‘karamu’ ya habari. Hakuna tena habari nyingine, “habari ya mji” ikawa heka heka na harakati za wanausalama kupambana na magaidi na waokozi kuokoa watu.

Sasa tazama picha hizo za awali za majeruhi ambao wanaonekana kuokolewa na polisi, halafu linganisha na maneno haya ya wanahabari kwamba:

“People covered in blood, were led out of the complex by police. Things are not good. People are dying."

Ufupi wa maneno ni kwamba, taarifa za BBC, AF, Agence France-Presse (AFP), Reuters news agency na vyombo vingine vya habari, vikidai kuwa hali ni mbaya watu wanakufa huku wengine wakiokolewa wakiwa wamelowa damu, zilikuwa zikipingana kabisa na kilichokuwa kikionyeshwa ‘mubashara’ (live).

Vyombo hivyo vikielezea namna shambuilio lilivyofanyika vikadai kuwa kulifika gari katika eneo la hoteli hiyo likiwa na milipuko ikalipuka na kisha waliolipua wakaanza kupiga watu risasi ovyo.

“Heavily armed men were firing indiscriminately, using bombs and automatic rifles to kill.”

Vyombo vya habari viliripoti kuwa washambuliaji walikuwa wamejizatiti kwa silaha madhubuti wakawa wanapiga risasi na kurusha mabomu ovyo.

Sasa vuta tu fikira mahali ambapo ‘magaidi’ wenye silaha nzito na mabomu wanarusha risasi na mabomu ovyo, kisha vuta hiyo fikira sasa tazama hizo ‘clips’ nilizotaja hapo juu uone hali ya watu waliokuwa katika tukio ambapo tunaambiwa:

It is terrible. What I have seen is terrible. Heavily armed men were firing indiscriminately, using bombs and automatic rifles to kill. The pictures that have been coming from inside are truly horrific. Ordinary people going about their business, murdered as they had lunch or did their jobs.”

Vyombo vya habari vinadai kumnukuu mtu mmoja akiitwa Charles Njenga akiwa katika eneo la tukio akidai kwamba aliona hali ya kutisha watu wenye silaha wanauwa watu ovyo waliokuwa wakijipatia chakula cha mchana au wakiwa wanaendelea na kazi zao.

Cha ajabu katika hali hiyo ya mtafaruku, magaidi wanauwa watu ovyo, vyombo vya habari vikaonyesha mama ntilie mmoja (mama lishe) kaleta sufuria la wali polisi wenye silaha wamepanga foleni wanapakuliwa wali wanakula. Mama huyo anajieleza kuwa aliona ni bora na yeye atoe mchango wake katika kupambana na magaidi hao. Na kwa sababu hawezi kushika bunduki, basi akaona ‘apambane’ kwa kuwapa chakula askari!?? Vyombo vya habari vikamsifia kwa “uzalendo”!!

Kweli mzalendo jasiri! Baada ya kutoa maelezo namna shambulio lilivyokuwa la kutisha na la kinyama, haraka haraka ikadaiwa kuwa kundi la al-Shabab limesema kuwa linahusika na shambulio hilo. Habari hiyo ikajaziwa nyama kwamba hao ni Al-Shabaab-The Somalia-based Islamic Extremist Group, ambao walifanya shambulio la kigaidi Westgate Mall mwaka 2013 na kuuwa watu 67.

Taarifa ya msemaji wa jeshi la Polisi, Kenya Joseph Boinnet ikadai kuwa waliolipua gari walikuwa ni magaidi wa kujitoa muhanga kwa hiyo walijilipua wenyewe wakafa ndani ya gari walilokuwa wamebeba mabomu.

Awali Polisi walisema kuwa hawajajua ni watu wangapi wamekufa, hata hivyo wakasema kuwa maiti zilikuwa zimezagaa katika mgahawa wa hoteli, kwenye ngazi za jengo na ndani ya ofisi, lakini wakaishia kusema kuwa kutokana na kwamba magaidi wanaendelea kushambulia: “There was no time to count the dead.” Kwa maana kuwa hapakuwa na muda wa kuhesabu maiti. Lakini mtoa habari mwingine wa polisi ambaye hakutaka kutajwa jina lake akasema kuwa:

“Maiti 15 zimepelekwa mochwari huku ikikisiwa kuwa zaidi ya watu 47 wameuliwa.”

Kama ilivyokuwa kwa Tanzania, hivi karibuni serikali ya Marekani ilikuwa imeonya kuwa Kenya kutakuwa na shambulio la kigaidi. Lakini wakati huo huo imedaiwa kuwa picha za kamera za usalama zimefichua kwamba kulikuwa na kikosi maalum cha Marekani ndani ya Kenya ambacho kipo kwa ajili ya kupambana na wanaodaiwa kuwa “Waislamu Siasa Kali” na “Al Shabaab”.

Taarifa zinasema kwamba, katika tukio la Jumanne, kamera zilinasa picha ya askari mmoja wa kikosi maalum-US Navy SEAL ambacho kipo Kenya katika operesheni za siri za kupambana na magaidi.

Mwaka 2013 lilipotokea shambulio la kigaidi Nairobi katika jumba la kibiashara Westgate, baadhi ya taarifa za magazeti zilimnukuu Rais Uhuru Kenyatta akiwalaumu makachero wa Marekani na Israel kwamba ndio waliosababisha shambulio hilo. Hoja ya Rais Uhuru ilikuwa kwamba, Serikali yake imeweka usalama wa nchi ya Kenya katika mikono ya makachero hao wa Marekani na Israel. Sasa walikuwa wapi mpaka Al Shabaab wakafanikiwa kufanya shambulio hilo kubwa? Rais Uhuru akaendelea kuhoji, mbona wataalamu hao wa Israel na Marekani nao wamekuwa kizani kama makachero wa Kenya mpaka wamepigwa?

He (President Uhuru Kenyatta) said he had counted on them for a heads-up to thwart an attack, instead of which both the Americans and Israelis were as much in the dark as his own security agencies.” (Tazama: Kenya blames US, Israeli intelligence for no heads-up on Nairobi attack.)

Hata hivyo, wakati shutuma hizo za Rais Uhuru na watu wengine zikichukuliwa tu kwamba ni ‘uzembe’ wa makachero wa Marekani na Israel au kuzidiwa ‘ujanja’ na Al Shabaab, wachambuzi wengine wanachimba zaidi wakiibuka na maswali yasiyojibika kwa majibu mepesi. Mfano katika tukio la 2013 inaelezwa kuwa baadhi ya watu walipewa tahadhari na jamaa zao waliopo ndani ya Idara ya Usalama ya Kenya- Kenya’s National Intelligence Agency (NIS), kwamba wasitembelee japo kupita kwa mbali katika nyumba la Westgate Shopping Mall. Kwa mujibu wa habari ya gazeti la Independent la Uingereza la tarehe 27 Septemba, 2013, baadhi ya maafisa wa NIS walitoa tahadhari kwa ndugu zao. Taarifa ya Independent ikamnukuu polisi mmoja wa kike ambaye wakati akihojiwa alisema kuwa yeye alikuwa amepewa taarifa na kaka yake ambaye ni afisa wa NIS kwamba siku ile ya Jumamosi siku lilipotokea shambulio asije kupita Westgate kwa sababu hataweza kukimbia. Independent walisema:

“A pregnant policewoman was warned by her brother, an NIS officer, not to visit Westgate. She has told police that her brother who is a NIS officer warned her not to visit Westgate that Saturday because she would not be able to run.”

Taarifa hizo zilichapishwa pia katika gazeti la The Star. Swali ni je, NIS walijua kwamba kutatokea shambulio? Na kama walijua, kwa nini hawakutoa taarifa ya wazi kwa wananchi wote? Lakini muhimu zaidi, kwa nini hawakuchukua hatua za kuzuiya? (Tazama: Some Got Warning To Avoid Westgate Before Bloody Siege: NIS officials told family members not to visit shopping mall.)

Katika kutafakari zaidi, wachambuzi hao wanarejea nyuma katika shambulio la kigaidi katika Balozi za Marekani kule Nairobi na Dar es Salaam mwaka 1998, wakisema kuwa mtuhumiwa mkuu (mastermind and coordinator) alitajwa kuwa ni Ali Mohamed aka Ali “the American”. Katika kesi akitajawa kama “point man”. Huyu alikamatwa na makachero wa Marekani miaka miwili baada ya shambulio na ikathibitishwa kuwa ni mmoja wa watuhumiwa wakuu.

Hata hivyo inaelezwa kuwa ‘mshambuliaji huyu “Al Qaeda bomber” Mohamed, alipata mafunzo ya kijeshi katika chuo cha kijeshi Fort Bragg, North Carolina, na kisha kufanya kazi kama mtaalamu wa milipuko katika chuo kingine John F Kennedy Special Warfare Center and School mpaka mwaka 1989.

Kwa mtu aliyepitia mafunzo na nafasi hizo katika Idara nyeti za kiusalama za Marekani, inakuwa vigumu kuelewa anageukaje kuwa Al Qaida, kama si kufanya kazi hizo kwa kutumwa. Ndio pale mchambuzi mmoja kwa maoni yake akasema:

“Mohamed was of course, a double agent, a living proof to the symbiosis between the Jihadists and the U.S. intelligence community.”

Pengine itakuwa vyema nisijipe ufundi wa kutafsiri maoni yake hayo kwa Kiswahili. Niyaache kama yalivyo.

 

Most Read

  • Week

  • Month

  • All