Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Amani ya Stokholm, SIPRI, zaidi ya thuluthi moja ya silaha zilizonunuliwa duniani katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, zilinunuliwa kutoka Marekani na nusu ya silaha hizo zilitumwa katika eneo la Mashariki ya Kati.

 

Shirika hilo la kimetaifa limesema kuwa uuzaji wa silaha hizo uliongezeka kwa asilimia 15 ikilinganishwa na wa kipindi cha kati ya mwaka 2011 hadi 2015.

Kwa mujibu wa ripoti ya shirika hilo Marekani, Ufaransa na Ujerumani ambazo ni nchi tatu kubwa zinazouza silaha kwa wingi duniani, ziliongeza uhamishaji na mauzo ya silaha zao katika pembe tofauti za dunia.

Saudi Arabia ambayo ni nchi inayonunua silaha nyingi zaidi duniani, iliongeza kiwango cha ununuzi wake wa silaha kwa asilimia 61, nayo Qatar ikaongeza kiwango hicho kwa asilimia 36.

Hivi karibuni Emirates (UAE) nayo ilitiliana saini na Marekani mkataba wa kununua silaha zenye thamani ya dola bilioni 33 za Marekani, zikiwemo ndege za kivita 50 aina ya F35 na droni 18 zenye kusheheni mabomu.

Simon Wiesmann, mtafiti wa ngazi za juu katika taasisi ya SIPRI, amesema kwamba nchi kadhaa katika eneo la Asia na Pacific zinaichukulia mikakati ya kijeshi ya China kuwa tishio kwao, hivyo kuhalalisha mipango yao ya kujizatiti kwa silaha za kisasa.

Nchi za Kiarabu za Kusini mwa Ghuba ya Uajemi kama vile Saudi Arabia, Emirates, Bahrain na Qatar kila mwaka hutumia mabilioni ya dola kwa ajili ya kununua silaha kutoka Marekani.

Katika mwaka wa kwanza wa urais wa Donald Trump nchini Marekani, Saudi Arabia ilitiliana saini na nchi hiyo mkataba wa kununua silaha na zana za kivita zenye thamani ya mamia ya mabilioni ya dola.Parstoday.

 

Latest News

Most Read