Na Sheikh Ashraf Ibrahim Ashawadufy

Shukurani zote anastahiki Mwenyezi Mungu, Mola mlezi wa ulimwengu na kwake yeye tunaomba msaada, rehema na amani zimfikie Bwana wetu Muhamad (s.a.w).

Amani katika kamusi za lugha ni kwa maana ya salama na kuongoka, uaminifu na utulivu na kutokwa na khofu husemwa aliaminia amani naye ni Mwenyezi Mungu.

Mji wenye amani ni ule ambao watu wake wapo katika utulivu, na ameaminia shari na miongoni mwa hizo ni kusalimika na kuongoka. Basi amani ni kule kujisikia mtu amani na utulivu na kutokuwa na khofu kwa yale anayojitahadharisha nafsi yake au dini yake au heshima yake au mali yake na Qur’ani tukufu pale ilipotuzungumzia juu ya amani, imezungumza kwa sifa ya ujumla ya maana yake.

Amesema Mwenyezi Mungu mtukufu, (“Na kumbukeni khabari  hii pia) tulipoifanya nyumba ( ya Al Kaaba) iwe  mahali pa kuendewa na watu na mahali pa salama. Na mahali alipokuwa akisimama Ibrahim pafanyeni pawe pa kusali. Na tulimuusia Ibrahim na Ismail (Tukaawambia): “itakaseni (Isafisheni) nyumba yangu kwa ajili ya wale wanaoizunguka kwa ajili ya kutufu na wanaokaa hapo na ( kwa ajili ya) wanarukuu na kusujudu hapo pia.” Surat  Al-bakara aya ya (125).

Amesema tena Allah (s.w), “Na kama mmoja wenu amewekewa amana na mwingine, akimuamini basi aliyeaminiwa airudishe amana ya mwenzake, na amche mwenyezi mungu…………

…” Surat Al-bakara 283.

Hapana shaka kwamba amani ya nchi sio kanuni ambayo inaegemea amani yenye maana kuu, pindi amani ya nchi ndio msingi wa amani ya uchumi na jamii na viwanda na mengine mengi yale tunayopata dalili za kidini tumezunguza hapa awali juu ya amani ya nchi kama sababu miongoni mwa sababu za ukarimu wa umma juu ya hilo.

Amesema Mwenyezi Mungu mtukufu, “Na pale aliposema Ibrahim, Mola wangu mlezi ufanye mji huu uwe wa amani na uwaruzuku watu wake miongoni mwa matunda mwenye kuamini miongoni mwao, Imani, Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho.

Akasema na yule aliyekufuru, basi tutamstarehesha kidogo kisha tutampambanisha na adhabu ya moto na kisirani kilioje kurejea motoni” Surat Albakarat, aya ya 126.

Na hili ni fungamano baina aya, riziki na amani ametanguliza hapa ombi la amani kuliko riziki na uchumi, kwani hakuna uchumi kama kutakosekana amani.

Na amesema tena Mwenyezi Mungu katika Surat Ibrahim “Na hebu kumbuka pale aliposema Ibrahim mola wangu mlezi ufanye mji huu uwe wa amani na uniepushe mimi na watoto wangu tusiabudie masanamu mola wangu hakika hao wametupoteza sana watu basi mwenye kunifuata mimi huyo yupo pamoja na mimi atakaye niasi hakika yako ni msamehevu mwenye rehema mola wangu mimi nimeiweka familia yangu katika uchamungu lisilo kilimo katika nyumba yako tukufu mola wangu mlezi basi wasimamishe swala, na wajaalie watu kuwajia na uwaruzuku miongoni mwa matunda huwenda akashukuru” Surat Al-bakara  aya ya 37.

Katika qur-ani tukufu na imetaja pia katika Surat Qasas na Surat Ankabuti kwa wakati tunazikuta kwamba ufakiri umekusanyika na khofu katika msemo mmoja amesema Mwenyezi mungu mti ambao ulikuwa na amani na utulivu zinakuja riziki zake kwa wingi toka  kila mahala nao wakakufuru neema za Mwenyezi mungu na akawapambanisha Mwenyezi Mungu vazi la njaa na khofu kwa yale waliyoyafanya”  Surat Anahli  aya ya 112, na amesema tena Mwenyezi Mungu mtukufu “kwa ajili ya kuzoea makuraishi kuzoea kwao safari ya kusi na kaskazi basi muabuduni mola wa nyumba hii ambaye amewalisha wasipate njaa na akawasalimisha na khofu:” aya ya  -14-  Surat Kuraishi.

 Hapa ametanguliza kutaja njaa kuliko khofu kwani mwanzo mwa alama za khofu kwani hudhihiri katika njaa na ufakiri ambao unakuwa ni sababu yake kama ilivyokuwa alama za aman na bishara zake hudhihiri kwenye riziki na wingi wake na ukarimu kama sababu zake na mpaka hapa akapambanisha mtume (s.a.w) baina ya maisha bora ya binadamu na baina ya amani amesema mtume (s.a.w) yeyote atakaye amka na amani katika familia yake na afya ya mwili wake na ana chakula cha siku yake hii huyo ni kama amemiliki dunia nzima na vyote vilivyomo, akaanza mtume (s.a.w) kutaja alama za furaha ni amani kwani hakuna furaha wala raha wala maendeleo wala kufaulu kwa mtu mmoja na jamii isipokuwa na dola saba za viwanda vikubwa kama ilivyokuwa viwanda vyao na uzalishaji wao huenea duniani mashariki na magharibi na kupigana vita kwani uwezo wao wakiaskari ni mkubwa hutikisa bahari na mito ili kuhami uchumi wake kwa nguvu zake za kiaskari ili kuhakikisha amani na kuzalisha mali ilikueneza chakula na mavazi kwani kwa kufanya kazi ndio kupata maendeleo ya nchi.

 Kwa hayo basi kuitatua matitizo na kuwasogeza watu wake na kusaidia katika njia ya maendeleo yao basi umma hujengwa kwa kufanya kazi na kuzalisha mali, na huyu hapa ni mtume (s.a.w) hapana muislam yeyote atakayepanda mmea au kulima shamba, na akala mazao yake ndege au binadamu au mnayama isipokuwa yeye huandikiwa malipo ya sadaka” hapa mtume pale alipotazama hali ya hewa ya madina na muelekeo wake alimuomba Mwenyezi Mungu kutatua matatizo ya nchi yake na kueneza amani salama.

kuwahimiza watu juu ya kutembea na kuzalisha na katika sahihi mbili ndiyo hadithi hiyo hapo juu, na pia ameitoa Imam Twabar-ani toka kwa kaabi bin Ajrata amesema: alipita kwa mtume (s.a.w) mtu mmoja akawaona masahaba wa mtume (s.a.w) juu ya juhudi zao na harakati zao wakasema “Ewe mtume wa Mwenyezi mungu laiti ingekuwa haya katika njia ya Mwenyezi Mungu, akasema mtume (s.a.w) “Ikiwa mtu ametoka kwa ajili ya mtoto wake mdogo basi huyo yupo katika njia ya Mwenyezi Mungu na akiwa ametoka ili watu wamuone na kujifaharisha huyo yupo katika njia ya Shetani” .

Kama ilivyokuwa hapana budi kupambana na mawimbi ya uhalifu ambayo huvunja nchi kati ya nyakati na nyakati na hutumika katika kuwatisha uhai wa raia wake na kulenga kuwatia woga baina ya watu au kwa upande wa kuwaudhi au kuwatangazia maisha yao na kuwapeleka maisha.

Email : This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it._center