‘Ulinzi’ kikwazo kesi ya Mskh wa Uamsho

Ni kwa ajili ya kusomewa hati mpya ya Mashtaka

Wakili: Huenda Upelelezi umekamilika

Na Bakari Mwakangwale

SERIKALI imeshindwa kuwafikisha Viongozi wa Jumuiya ya Uamsho, Mahakamani Jijini Dar es Salaam, kutokana na kukosa ulizi wa kutosha.

Awali, kwa mujibu wa taarira zilizotufikia, zilieleza kuwa Jumatatu ya wiki hii (Agosti 10, 2020) Masheikh hao wangefikishwa Mahakama ya Kisutu Jijini Dar es Salam, kwa ajili ya kusoma hati mpya ya Mashtaka na kupokea taarifa kama upelelezi umekamilika.

Akiongea na Mwandishi wa Habari hizi, Wakili wa Masheikh hao Wakili Salim Abubakar, amesema upande wa wa mashtaka (serikali) uliiomba Mahakama kuwa, Masheikh hao wamefikishwe Mahakamani Jumatatu ya Agosti 17, 2020.

“Hawakuletwa Mahakamani na sababu walizozitoa ni kutokana na kukwama kwa mpangilio wa mambo ya Ulinzi na Usalama kwa ajili ya Masheikh kwa upande wa Serikali, hivyo waliomba Tarehe ya karibu wajipange kiulinzi ili waweze kuwaleta Mahakamani” Amesema Wakili Abubakar.

Kufatia mkwamo huo, Wakili huyo alisema hafahamu ni ulinzi wa aina gani unaohitajika kwafikisha Masheikh hao Mahakamani, kwani wapo watuhumiwa wenye kesi nzito za mauaji wano wanapata ulinzi wa kufikishwa Mahakamani.

“Masheikh tuhuma zao ni hizo, kwamba wameshiriki tuhuma za kigaidi, ambazo hazijawa wazi sasa hatujui ni ulinzi wenye uzito wa namana gani unaohitajika kwa ajili ya kuwafikisha Mahakamani, tofauti na ulinzi wanaokuja nao kila mara Mahakamani.” Amesema Wakili Abubakar.

Wakili Abubakar, alisema siku hiyo ya Jumatatu (wiki hii) Masheikh hao walikuwa wafikishwe kwa ajili ya kusomewa hati mpya ya Mashtaka na kuambiwa kama upelelezi umekamilika ili kesi sasa iende hatua nyingine, akasema kwa kauli hiyo mbele ya Maha kama, ni kama upelelezi wao umekamilika.

Alisema, baada ya kuelezwa sababu za kushindwa kufikishwa kwa wateja wao, na kuomba kuahirishwa alisema wao waliafiki nakuomba ipangwe tarehe ya karibu kwani, akasema wao hata wangeambiwa warudi siku ya pili wangerudi tu hivyo ilipangwa Agasti 17, 2020, ambapo upande wa utetezi uliafiki.

Latest News