Bi. Tasnim Nazeer, atakuwa ripota wa kwanza Muislamu kuonekana katika televisheni akiwa amevalia vazi la staha la Kiislamu la hijabu huko Scotland, Uingereza.
Nazeer ambaye ni mwenyeji wa Glasgow, alianza kuripoti katika televisehni ya STV News mapema wiki hii.
Amesema ana furaha kubwa kufanya kazi yake ya kwanza kama ripoti wa STV News, ambapo ripoti hiyo imehusu kusaidia familia ambazo zimekumbwa na msiba Scotland.
Amesema ana uhakika kuwa hakuna mwaname Muislamu aliyevalia hijabu aliyewahi kuripoti katika televisheni ya Scotland.
"Naishukuru STV kwa kunipa fursa hii na nina furaha kuwa imeajiri kwa msingi wa ujuzi na uwezo wangu wa kufanya kazi."
Amesema ni muhimu kwa vyombo vya habari Scotland kuwa na wafanyakazi ambao wana akisi taswira ya kitaifa ya jamii nzima ili mitazamo mbalimbali iweze kusikika. (IQNA).